Home » » HOT NEWS: WAZIRI MKUU AMWAGIZA MKUU WA MKOA KUPELEKA TIMU YA UCHUNGUZI ILI KUWABAINI WALIOKULA FEDHA ZA CHAMA CHA USHIRIKA CHA UKONONGO

HOT NEWS: WAZIRI MKUU AMWAGIZA MKUU WA MKOA KUPELEKA TIMU YA UCHUNGUZI ILI KUWABAINI WALIOKULA FEDHA ZA CHAMA CHA USHIRIKA CHA UKONONGO

 
Na  Walter   Mguluchuma,  Katavi  yetu blog

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amemtaka  Mkuu wa Mkoa wa Katavi , Meja
Generali Mstaafu , Raphael Muhuga kupeleka mara moja  timu ya wakaguzi
 wilayani Mlele  ili kuwabaini wote  waliofuja  fedha cha Chama Cha
Ushirika cha Ukonongo  ili hatua za kisheria ziweze  kuchukuliw dhidi
yao .

Alitoa agizo hilo  wakati akihutubia  mkutano wa  hadhara katika
kiwanja cha Inyonga  wilayani Mlele  uliohudhuriwa  na  umati  mkubwa
wa watu akisisitiza kuwa  watumishi  wafanye kazi zao  wakizingati
maadali  na kujiepusha na  tabia  ya ubadhifu  wa mali ya umma .

“Namwagiza Mkuu wa Mkoa wa Katavi (Muhuga)  kuhakikikisha anapeleka
timu ya wakaguzi  wilayani hapa haraka  iwezekanavyo  ili   wote
waliokula  fedha za Chama Cha Ushirika cha Ukonongo  wabainike na
kuchukuliwa  hatua za Kisheria “ aliagiza Wziri Mkuu Majaliwa .

Waziri Mkuu   alisisitiza  kuw kila mtumishi  awajibike   kwa
uaminifu na uadilifu  kulikangana na taaluma yake  ili  kuhkikisha
wananchi wanapata maenedelo  wanayostahiki .

“ Wahitajika  watumishi  wanaosikiliza maelekezo yanayotolewa na
Serikali  yao ….  Nayafanyia  kazi  kwa sababu   malengo ya Rais  John
Magufuli  ni  kueta mabadiliko nchini  ambaye hataweza  basi aandike
barua ya kuacha kazi “ alisisitiza .

Wakati huo  huo Waziri Mkuu  amesistiza kuwa Serikali ya  Awamu ya
Tano  imedhamiria  kumaliza ttizo sugu la upatikanaji wa umeme  nchini
 ambapo  imetenga zaidi ya Sh  trioni 1.0  kwa ajili ya kusambaza
nishati hiyo  nchini kote .

Waziri Mkuu  amehitimisha  leo  mchana  ziara yake  ya  kikazi ya siku
 nne  mkoani Katavi  kwa  kufanya mkutano  wa hadhara  kijijini
Majimoto  wilayani Mlele  kabla ya  kuelekea  mjini Namanyere
wilayani Nkasi  kuanza  ziara yake  ya siku  tatu  mkoani Rukwa.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa