Home » » ATAKAYEKATISHA MASOMO YA MTOTO WA KIKE KWA KUMPA MIMBA AU KUMUOA AKIWA MDOGO JELA MIAKA 30

ATAKAYEKATISHA MASOMO YA MTOTO WA KIKE KWA KUMPA MIMBA AU KUMUOA AKIWA MDOGO JELA MIAKA 30

 
Na  Walter  Mguluchuma .
              Katavi .
  Waziri  Mkuu wa   Serikali ya  Jamuhuri ya  Muungano  wa  Tanzania  Kassimu  Majaliwa  amesema  Serikali  ya   awamu ya tano  imejipanga  kuhakikisha  ina   kuwalinda watoto  wote wa kike  ili wamalze   masomo     yao  na  itawachulia  hatua watu wote wate ambao  watakao wakatisha masomo  wanafunzi wa  na  wale wazizi ambao  watakao waozesha na kuwaoza watoto wao .
 Agizo  hilo  alilitowa  hapo  jana   wakati  alipokuwa  akiwahutubia    wananchi  wa   Halmashauri ya  Manispaa  ya  Mpanda  wakati wa mkutano wa  hadhara  uliofanyika   katika   uwanja  wa  shule ya  Msingi ya  Kashaulili  Mjini  hapa .
  Alisema   Serikali   haiko   tayari  kuona  mtoto wa kike  anakatishwa  masomo  yake kwa  ajiri ya  kuolewa au kupata  ujauzito  watu  watambue kuwa   wanaofanya hivyo   adhabu yake ni kifungo  cha miaka 30 jela .
 Aliwaonya watu  wale  ambao  wamekuwa  na  tabia ya kuwasemesha na  kuwasalimia  mara  mbilimbili  wanafunzi wa kike kwa   lengo  la  kutaka  kuwa  nao na  mahusiano ya  kimapenzi .
 Majaliwa   alieleza  kuwa   Serikali  haita  sita  kuwachulia  hatua  watu  wato  ambao  watawakatisha  masomo watoto wa  kike  na wale wazazi ambao   watawaoza na  kuwaolesha  watoto  wao  wanafunzi .
 Alisema  wapo baadhi ya  wazazi  ambao  watoto wao wakike  ni  wanafunzi     wamekuwa  wakiolewa  na  kuowa  bila  ridhaa  yao watoto  wao .
Majaliwa  alisisitiza  kuwa   Serikali   itahakisha  inawachukulia  hatua  wazazi wanaowaza watoto wao  wa kike na  wazazi  ambao wanao  wasindikiza  watoto wao  kwenda kuowa .
Alisema  watu lazima  watambue  kuwa  mtoto wa  mwenzako ni  mtoto  wako  kama   ambavyo   kauli y  mbiu  ya  mke  wa  Rais  wa  awamu  ya  nne  alivyokuwa   akiisisitiza .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa