Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya tano imejipanga kuhakikisha ina kuwalinda watoto wote wa kike ili wamalze masomo yao na itawachulia hatua watu wote wate ambao watakao wakatisha masomo wanafunzi wa na wale wazizi ambao watakao waozesha na kuwaoza watoto wao .
Agizo hilo alilitowa hapo jana wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi ya Kashaulili Mjini hapa .
Alisema Serikali haiko tayari kuona mtoto wa kike anakatishwa masomo yake kwa ajiri ya kuolewa au kupata ujauzito watu watambue kuwa wanaofanya hivyo adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 jela .
Aliwaonya watu wale ambao wamekuwa na tabia ya kuwasemesha na kuwasalimia mara mbilimbili wanafunzi wa kike kwa lengo la kutaka kuwa nao na mahusiano ya kimapenzi .
Majaliwa alieleza kuwa Serikali haita sita kuwachulia hatua watu wato ambao watawakatisha masomo watoto wa kike na wale wazazi ambao watawaoza na kuwaolesha watoto wao wanafunzi .
Alisema wapo baadhi ya wazazi ambao watoto wao wakike ni wanafunzi wamekuwa wakiolewa na kuowa bila ridhaa yao watoto wao .
Majaliwa alisisitiza kuwa Serikali itahakisha inawachukulia hatua wazazi wanaowaza watoto wao wa kike na wazazi ambao wanao wasindikiza watoto wao kwenda kuowa .
Alisema watu lazima watambue kuwa mtoto wa mwenzako ni mtoto wako kama ambavyo kauli y mbiu ya mke wa Rais wa awamu ya nne alivyokuwa akiisisitiza .
No comments:
Post a Comment