Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa amewaagiza wakuu wa Wilaya wote hapa Nchini kuhakikisha watu wote wanao waongoza wanafanya kazi na Serikali haita kubali wala haitaki kusikia Mkuu wa Wilaya analia njaa kwenye Wilaya yake ..
Agizo hilo alilitowa hapo juzi wakati alipokuwa akiongea na watumishi wa Halmashauri zote tano za Mkoa wa Katavi pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali na viongozi wa dini katika Ikulu ya Mpanda .
Alisema Serikali haitaki kusikia Mkuu wa Wilaya analia njaa kwenye Wilaya yake kutokana na uzembe wa watu wake kutofanya kazi na kutolima hivyo wakuu wa Wilaya wanao wajibu wa kuwasimamia watu wao wafanye kazi .
Alisema kila Mkuu wa Wilaya hapa Nchini kwenye Wilaya yake ahakikishe anawawahamasisha wananchi wake walime ili waweze kujitoshereza kwa chakula kwenye maeneo yao .
Alisisitiza kuwa Serikali itapeleka msaada wa chakula kwenye Wilaya ambayo imepata upungufu wa chakula kutokana na sababu ile ambayo haizuiliki kama vile hari ya ukame na sivinginavyo .
Alieleza Serikali imepanga na itahakikisha pembeo za kilimo zinawawafikia wakulima kwenye maeneo yao kabla ya miezi miwili ya kuanza kwa msimu wa kilimo .
Kwa upande wa watumishi aliwataka watambue kuwa wao ni watumishi wa Wantania hivyo wanakiwa kuwahudumia watu kwa kuwapokea na kuwasikiliza na kuwahudumia .
Alisema Serikali ya awamu ya tano inasisitiza uwajibikaji inataka watumishi wote hapa nchi wafanye kazi na wabadilike katika utendaji wao wa kazi na kila mtumishi anakuwa mwadilifu .
Majaliwa alieleza Serikali imeongeza bajeti ya fedha za maendeleo kutoka asilia 27 hadi kufikia asilia 40 hivyo fedha watumishi wanakiwa kuwa waminifu wa kusimamia fedha hizo .
Hivyo aliwaka madiwani kuhakikisha wanasimamia fedha hizo kwenye Halmashauri zao na miradi inayo jengwa inalingana na fedha zilzopokelewa na miradi inajengwa kwa ubora unao lingana na fedha .
Awali Mkuu wa Mkoa wa Katavi wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga alisoma taarifa ya maendeleo ya mkoa huo ambapo alisema Mkoa wa Katavi umeandaa mazingira ya uwekezaji ili wananchi wake waondokane na umasikini ifikiapo mwaka 2026.
Alisema Mkoa wa Katavi unakabiliwa na baadhi ya changamoto mbalimbali ikiwemo ya Mkoa huo kutokuwa na Hospitali ya Mkoa .
Changamoto nyingine ni tatizo la umeme kukatika mara kwa mara kutokana na uchakavu wa jenereta za mashine ambazo kabla ya kuletwa Mkoani Katavi mwaka 1993 zilikuwa zimeisha tumika Mkoani Shinyanga kwa kipindi cha miaka kumi.
No comments:
Post a Comment