Na Walter Nguluchuma .
Katavi
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imewawahukumu watu wane kifungo cha jumla ya miaka 60 jela baada ya kupatikana na hatia ya kukamatwa na meno ya Tembo vipande 25 vyenye uzito wa kilogramu 46 ya thamani ya Tsh Milioni 371,600,000
Hukumu hiyo ilitolewa hapo jana na Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa baada ya Mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka .
Washitakiwa waliohukumiwa kifungo hicho ni Justine Baruti 39 Mkazi wa Kijiji cha Ivungwe Makazi ya Katumba Wilaya ya Mpanda, Bonifaphace Hoza 40 , Elias Hoza 46 wakazi wa Kijiji cha Kalela Kasulu Mkoa wa Kigoma na Credo Gervas 45 Mkazi wa Kijiji cha Ndurumo Makazi ya Wakimbizi ya Katumba .
Katika kesi hiyo upande wa mashitaka uliongozwa na wakili wa Seriali wa Mkoa wa Katavi Wakyo Simoni na ulikuwa na mashahidi 15 na washitakiwa walikuwa wakitetewa na wakili Elias Kifunda na washitakiwa hawakuwa na mashahidi wowote zaidi yao .
Awali katika kesi hiyo mwendesha mashitaka mwanasheria wa serikali Wakyo Simo alidai mahakamani hapo kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo hapo Desemba 24 2014 huko katika stendi kuu ya mabasi yaendayo Mikoani katika Mtaa wa Mji mwema Manispaa ya Mpanda .
Ilidaiwa na Mwendesha mashitaka huyo kuwa siku hiyo ya tukio Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi na Askari polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa washitakiwa hao wamepanga kusafirisha meno ya Tembo kuyatoa Mpanda na kuyapeleka Mkoani Kigoma kwa kutumia basi la Kampuni ya Adventure Connection Bus.
AliIambia Mahakama kufuatia tarifa hizo Askari wa Tanapa na Polisi walifika kwenye eneo hilo la stendi ya mabasi ambapo waliweza kuwashika washitakiwa wakiwa na meno hayo ya Tembo vipande 46 ndani ya basi la Kampuni ya Adventure
Mwanasheria huyo alidai kuwa mshitakiwa wa kwanza Justine Baruti siku hiyo ya tukio alishikwa na meno ya Tembo vipande 18 vyenye uzito wa kilogramu 33 yenye thamani ya Tsh milioni 249,600,000 na mshitakiwa wa pili Boniphace Hoza alishikwa na Meno ya Tembo vipande 7 yenye uzito wa kilogramu 13 yenye thamani ya Tsh milioni 124,000,000 wakiwa wameyapakia kwenye basi la Kampuni ya Adventure Connection.
Akisoma hukumu hiyo hapo jana Hakimu Chiganga Ntengwa alisema mahakama pasipo mashaka yoyote imewaona washitakiwa wanayo makosa yaliyowatia hatiani kulingana na ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo .
Hivyo watuhumiwa wa kwanza hadi wane Mahakama imewahukumu kifungo cha miaka mitano jela kwa kila mmoja kwa kosa la kuhusika kuhujumu uchumi na mshitakiwa wa kwanza Justine Baruti na mshitakiwa wa pili Boniphace Hoza walihukumi tena kila mmoja kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la kupatika na nyara za serikali na adhabu hizo zinakwenda kwa wakati mmoja .
Mahakama hiyo pia ilimwachia huru mshitakiwa wa tano Sadock Masamba katika kesi hiyo baada ya upande wa mashita kushindwa kutowa ushahidi wa wa kumtia hatiani mshitakiwa .
No comments:
Post a Comment