Sunday, August 21, 2016

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATOA AGIZO LA KASAKWA KWA RAIA WA BURUNDI WANAO INGIA KINYEMELA MKOANI KATAVI .


             Na  Walter  Mguluchuma .
                    Katavi .
  Waziri  Mkuu  wa  Jamuhuri  ya  Muungano wa Tanzania  Kassimu   Majaliwa  ameiagiza  kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Katavi inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Meja Generali Mstaafu   Raphael  Muhuga  hukakikisha inafanya ukaguzi  wa mara kwa mara kwenye Makazi ya Wakimbizi  ya  Katumba na  Mishamo ili kuwabaini  Raia wa  Burundi  wanao ingiza  kwenye  makazi hayo na kuishi bila kufuata  utaratibu wa  Nchi ya Tanzania .
 Majaliwa  alitowa  agizo  hilo  hapo  juzi wakati wa ziara yake ya  siku ya  kwanza  Mkoani  Katavi  alipokuwa  akiwahutubia     viongozi wa  Mkoa wa  Katavi  na  Wilaya  zote za  Mkoa huo katika  Ikulu  ndogo ya  Mpanda .
 Alisema wapo   Raia wa    Nchi   ya  Burundi  ambao  wamekuwa  wakiingia Mkoani  Katavi na kufikia  kwenya  Makazi ya  Wakizi ya  Katumba  Wilaya  ya  Mpanda  na   Makazi  ya  wakimbizi ya  Mishamo   wilaya    mpya  ya  Tanganyika  bila kufuata  kufuata utaratibu  kitu  ambacho ni hatari kwa usalama wa  nchi .
 Aliwaonya  waliokuwa  Raia  wa  Nchi ya  Burundi    waliopewa  Uraia wa  Tanzania  hapo   hapo  mwaka  jana  wanao ishi   katika  Makazi ya  Wambizi ya  Katumba  na  Mishamo kuacha  tabia ya   kuwapokea na kuwahifadhi  Raia  wa  Nchi ya  Burundi wanao  ingia   Nchini  bila kufuata  utaratibu wa  Nchi .
 Alisema wapo  Rai wa  Nchi ya  Burundi   ambao  wamekuwa  wakiingia   Nchini  kinyemela kwa kuwatumia  ndugu  zao wanaoishi  kwenye  makazi  hayo  waliopewa  Uraia wa  Tanzania na  kuingiza  silaha  kinyume cha  sheria na  kusababisha uharifu  na  ujangili wa  wanyama katika  Hifadhi ya  Taifa ya  Katavi .
Waziri  Mkuu Majaliwa  aliwakata   Raia  hao wapya  kuacha  tabia  hiyo ya  kuwaita  ndugu zao walioko  Burundi  kuja    kwenye  makazi  hayo  bila  kufuata   sheria  na  Taratibu  za   Nchi ya  Tanzania .
 Alisema   baada  ya  Serikali ya  Tanzania kuwapatia  Urai waliokuwa  Raia wa  Burundi  baadhi yao  wamegombea  nafasi  mbalimbali za uongozi  na  kupewa  dhamana  hiyo na  wameanza  kuitumia  vibaya   dhamana  hiyo ya uongozi  
Alieleza  kuwa  viongozi  hao  wameanza  kutumia  nafasi  hizo za  uongozi  kuwaingiza  watu  kutoka  Burundi na  wao  ndio wamekuwa watetezi  wao wakubwa na kuwasemea  pindi  wanapokuwa  wamekamatwa .
 Majaliwa  alisisitiza  kuwa  endapo  wataendelea  na  tabia  hiyo  Serikali  haita  sita kutowa  uamuzi  mwingine  kwa  waliokuwa  Raia wa  Burundi  ambao  wamepewa  uraia wa  Tanzania .
Aliwaka  Raia  hao  wapya  kujenga  utaratibu wa kujilinda  wao  wenyewe ili  waweze  kuwabaini watu wanao  ingia  kiholela  na   kuingiza  silaha  kinyume  cha  utaratibu .
Kutokana  na  hari  hiyo  naingiza   kamati ya ulinzi na  usalama ya  Mkoa wa  Katavi kufanya  ukaguzi wa  mara kwa  mara  kwenye  Makazi hayo ya  Katumba  na  Mishamo    ilikuwabaini  na kuwakamata    watu  wote  wanatoka  nje ya  nchi na kuingia  kwenye  makazi  hayo  bila  kufuata  utaratibu  aliagiza   Waziri  Majaliwa
Awali  Mkuu wa  Mkoa  wa   Katavi   Meja  Generali  Mstaafu  Raphael  Muhaga  katika   taarifa  yake  aliyoisoma kwa   waziri  Mkuu     Majaliwa  alieleza  kuwa  kwa  mujibu wa  Sensa  iliyofanyika   mwaka   2007 ya  Wakimbizi  katika  makazi  hayo  wakimbizi  160,000 waliomba  Uraia wa  Tanzania .
Na  baadhi yao walishindwa kupata  uraia  kutokana  na  sababu  mbalimbali  na  wengine  walirudi  Nchini  kwao  Burundi  kwa  hiyari yao  wenyewe

No comments:

Post a Comment