Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa ameiagiza kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Katavi inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga hukakikisha inafanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye Makazi ya Wakimbizi ya Katumba na Mishamo ili kuwabaini Raia wa Burundi wanao ingiza kwenye makazi hayo na kuishi bila kufuata utaratibu wa Nchi ya Tanzania .
Majaliwa alitowa agizo hilo hapo juzi wakati wa ziara yake ya siku ya kwanza Mkoani Katavi alipokuwa akiwahutubia viongozi wa Mkoa wa Katavi na Wilaya zote za Mkoa huo katika Ikulu ndogo ya Mpanda .
Alisema wapo Raia wa Nchi ya Burundi ambao wamekuwa wakiingia Mkoani Katavi na kufikia kwenya Makazi ya Wakizi ya Katumba Wilaya ya Mpanda na Makazi ya wakimbizi ya Mishamo wilaya mpya ya Tanganyika bila kufuata kufuata utaratibu kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa nchi .
Aliwaonya waliokuwa Raia wa Nchi ya Burundi waliopewa Uraia wa Tanzania hapo hapo mwaka jana wanao ishi katika Makazi ya Wambizi ya Katumba na Mishamo kuacha tabia ya kuwapokea na kuwahifadhi Raia wa Nchi ya Burundi wanao ingia Nchini bila kufuata utaratibu wa Nchi .
Alisema wapo Rai wa Nchi ya Burundi ambao wamekuwa wakiingia Nchini kinyemela kwa kuwatumia ndugu zao wanaoishi kwenye makazi hayo waliopewa Uraia wa Tanzania na kuingiza silaha kinyume cha sheria na kusababisha uharifu na ujangili wa wanyama katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi .
Waziri Mkuu Majaliwa aliwakata Raia hao wapya kuacha tabia hiyo ya kuwaita ndugu zao walioko Burundi kuja kwenye makazi hayo bila kufuata sheria na Taratibu za Nchi ya Tanzania .
Alisema baada ya Serikali ya Tanzania kuwapatia Urai waliokuwa Raia wa Burundi baadhi yao wamegombea nafasi mbalimbali za uongozi na kupewa dhamana hiyo na wameanza kuitumia vibaya dhamana hiyo ya uongozi
Alieleza kuwa viongozi hao wameanza kutumia nafasi hizo za uongozi kuwaingiza watu kutoka Burundi na wao ndio wamekuwa watetezi wao wakubwa na kuwasemea pindi wanapokuwa wamekamatwa .
Majaliwa alisisitiza kuwa endapo wataendelea na tabia hiyo Serikali haita sita kutowa uamuzi mwingine kwa waliokuwa Raia wa Burundi ambao wamepewa uraia wa Tanzania .
Aliwaka Raia hao wapya kujenga utaratibu wa kujilinda wao wenyewe ili waweze kuwabaini watu wanao ingia kiholela na kuingiza silaha kinyume cha utaratibu .
Kutokana na hari hiyo naingiza kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Katavi kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye Makazi hayo ya Katumba na Mishamo ilikuwabaini na kuwakamata watu wote wanatoka nje ya nchi na kuingia kwenye makazi hayo bila kufuata utaratibu aliagiza Waziri Majaliwa
Awali Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhaga katika taarifa yake aliyoisoma kwa waziri Mkuu Majaliwa alieleza kuwa kwa mujibu wa Sensa iliyofanyika mwaka 2007 ya Wakimbizi katika makazi hayo wakimbizi 160,000 waliomba Uraia wa Tanzania .
Na baadhi yao walishindwa kupata uraia kutokana na sababu mbalimbali na wengine walirudi Nchini kwao Burundi kwa hiyari yao wenyewe
0 comments:
Post a Comment