Na Walter Mguluchuma, Katavi
yetu blog
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Katavi , Meja
Generali Mstaafu , Raphael Muhuga kupeleka mara moja timu ya wakaguzi
wilayani Mlele ili kuwabaini wote waliofuja fedha cha Chama Cha
Ushirika cha Ukonongo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliw dhidi
yao .
Alitoa agizo hilo wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika
kiwanja cha Inyonga wilayani Mlele uliohudhuriwa na umati mkubwa
wa watu akisisitiza kuwa watumishi wafanye kazi zao wakizingati
maadali na kujiepusha na tabia ya ubadhifu wa mali ya umma .
“Namwagiza Mkuu wa Mkoa wa Katavi (Muhuga) kuhakikikisha anapeleka
timu ya wakaguzi wilayani hapa haraka iwezekanavyo ili wote
waliokula fedha za Chama Cha Ushirika cha Ukonongo wabainike na
kuchukuliwa hatua za Kisheria “ aliagiza Wziri Mkuu Majaliwa .
Waziri Mkuu alisisitiza kuw kila mtumishi awajibike kwa
uaminifu na uadilifu kulikangana na taaluma yake ili kuhkikisha
wananchi wanapata maenedelo wanayostahiki .
“ Wahitajika watumishi wanaosikiliza maelekezo yanayotolewa na
Serikali yao …. Nayafanyia kazi kwa sababu malengo ya Rais John
Magufuli ni kueta mabadiliko nchini ambaye hataweza basi aandike
barua ya kuacha kazi “ alisisitiza .
Wakati huo huo Waziri Mkuu amesistiza kuwa Serikali ya Awamu ya
Tano imedhamiria kumaliza ttizo sugu la upatikanaji wa umeme nchini
ambapo imetenga zaidi ya Sh trioni 1.0 kwa ajili ya kusambaza
nishati hiyo nchini kote .
Waziri Mkuu amehitimisha leo mchana ziara yake ya kikazi ya siku
nne mkoani Katavi kwa kufanya mkutano wa hadhara kijijini
Majimoto wilayani Mlele kabla ya kuelekea mjini Namanyere
wilayani Nkasi kuanza ziara yake ya siku tatu mkoani Rukwa.

No comments:
Post a Comment