Na Walter Mguluchuma .
Katavi yetu Blog
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepanga kutengeneza barabara kwa kiwango cha Rami zitakazo uunganisha Mkoa wa Katavi na Mikoa mingine inayopakana na Mkoa huo .
Kauli hiyo ya Serikali ilitolewa hapo juzi na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa wakati alikuwa akiwahutubia Maefu ya Wanachi wa Kata ya Majimoto Wilayani Mlele kwenye uwanja wa Maji moto.
Majaliwa alisema Mkoa wa Katavi upo kwenye mpango wa kuunganishwa na mikoa mingine kwa barabara zake zote zina zinazoungana na Mkoa huo kutengenezwa kwa kiwango cha lami .
Alizitaja barabara hizo kuwa ni Mpanda Sumbawanga ambayo teyari ujenzi wake umeishaanza ,Mpanda Tabora ambapo taratibu za kuwapata wakandarasi zimeanza kufanyika na Mpanda Uvinza ambapo mkandarasi wa kutengeneza kilometa 32 za kuanzia Mpanda kuelekea Uvinza Mkoani Kigoma amekwisha patikana na anatarajia kuanza kazi hivi karibuni .
Waziri Mkuu Majaliwa aliwaeleza Wananchi hao kuwa kwa sasa Serikali ya Tanzania inayo inazo fedha za kutosha baada ya kuwabana mafisadi na wafanya biashara ambao wanao kwepa kulipa kodi .
Hari hiyo ya ukusanyaji mkubwa wa mapato ya Serikali imefanya Serikali ipange mipango yake ya maendeleo vizuri kutokana na kodi mbalimbali zinazokusanywa .
Alieleza kuwa Serikali imepanga pia kujenga Reli itakayotoka Mpanda hadi Karema kwa lengo la kufarisha mizigo kwa njia ya Treni kutoka Tanzania hadi Kongo kwa kupitia bandali ya Karema katika ziwa Tanganyika .
Pia alisema Serikali inampango wa kufungua furusa za utalii katika Mkoa wa Katavi na ndio maana wanatengeneza miundo mbinu ya uhakika ili watalii waweze kufika huku kwa urahisi .
Nae Mbunge wa jimbo la Kavuu Dk Pudensiana Kikwembe aliiomba Serikali iweza kuwapatia wanachi wa jimbo hilo maji safi na salama kwani robo tatu ya wananchi wa jimbo hilo hawapati huduma ya maji .
Alisema hata hao roba ya wakazi wa jimbo hilo wanao pata huduma ya maji sio safi wala salama hari ambayo imekuwa ikiwasababishia kupata mlipuko wa magonjwa mbalimbali .
No comments:
Post a Comment