Picha mbalimbali wakati wa kuapishwa leo kwa wakuu wa Wilaya ya
Mpanda Liliani Matinga, Mkuu wa Wllaya Mpya ya Tanganyika
Salehe Muhando na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Lecho Kasanda wakuu
hao wa wilaya wameapishwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja
jenerali mstaafu Raphael Muhuga katika Ikulu ndogo ya Mpanda
Picha na Walter Mguluchuma Katavi yetu blog
Picha na Walter Mguluchuma Katavi yetu blog
Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu Blog
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu jana amewaapisha wa kuu wa Wilaya watatu wa Wilaya z a Mkoa wa Katavi katika sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Ikulu ndogo ya Mpanda iliyoko katika maeneo ya Mtaa wa Kawajense .
Wakuu hao wa Wilaya walioapishwa ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Liliani Matinga, Mkuu wa Wilaya ya Mlele Lecho Kasanda na Mkuu wa Wilaya mpya ya Tanganyika Salehe Muhando .
Mara baada ya kuapishwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi aliwapatia maagizo mbalimbali wakuu hao wapya wa Wilaya kwa ajiri ya utekelezaji wa majukumu ya kazi ya ukuu wa Wilaya .
Baadhi ya maagizo aliyowapatia ni wahakikishe wasifanye jambo lolote kwenye Wilaya zao ambalo linaweza kuharibu kilimo .
Pia wakuu hao wa Wilaya amewataka wadumishe ufaulu wa wanafunzi kutoka na mkoa huo kufanya vizuri kwa ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba kwa miaka miwili mfululizo za 2014 na 2015
Pia aliwaagiza wawe wasimamizi wa fedha za Halmashauri zao na lazima wajue miradi yote ilioko katika Halmashauri na kuikagua kama ipo kwenye kiwango kinachotakiwa .
Rc Muhuga alisema Mkoa wa Katavi unakabiliwa na changamoto ya wafugaji wanao hamia kiholela kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa huku wakiwa hawana vibali na wamekuwa wakivamia bunga ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi na vyanzo vya maji pamoja na kukata miti ovyo .
Mkuu Mpya wa Wilaya ya Tanganyika alihaidi kuwa atahakikisha anafanya kazi usiku na mchana na atajitahidi kuondoa changamoto zitakazo kuwa zinawakabili wananchi wake hasa za huduma ya jamii .
Nae DC wa Mlele Lecho Kasanda alisema atahakikisha kwenye Wilaya yake swala la watumishi hewa linakuwa ndoto katika Wilaya ya Mlele kwani taarifa alizopata Wilaya hiyo ilibainika kuwa na watumishi hewa kumi na moja .
Nae Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Liliani Matinga alisema atahakikisha anasimamia uboreshwaji wa elimu ili wanafunzi waweze kufaulu katika ufaulu wa juu.
0 comments:
Post a Comment