Bwana James akiwa amefungwa kamba baada ya kushindwa kulipa Deni la Tsh 30,000
Bwana James akiwa bado kifungoni kwa kushindwa kulipa Deni la Tsh 30,000
Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu blog
Katika hari ambayo haikutarajiwa katika makaburi ya Kawajense Manispaa ya Mpanda Mkazi wa mtaa wa Kigamboni James Jamesi amejikuta akifungwa kamba ya naironi miguuni na mikoni makaburini wakati wa mazishi ya Elias Kasiguru baada ya kushindwa kulipa fedha alizotakiwa kulipa na watani wa kabila lake na kusababisha ibada iliyokuwa ikiongozwa na padre Maliseli Butoyi isimame kwa zaidi ya dakta 20.
Tukio hilo la aina yake katika mji wa Mpanda lilitokea hapo jana majira ya saa kumi na mbili jioni katika maburini ya Kawajense ya waumini wa dhehebu la Romani Katoliki.
Katika tukio hilo ambapo James alikuwa ni rafiki wa karibu wa marehemu Elias Kasigulu aliamuru mwili wa marehemu hiyo usiingizwe ndani ya kaburi kwa ajiri ya mazishi mpaka hapo atakapo kuwa amepewa kiasi cha shilingi elfu kumi agizo ambalo lilitekelezwa na mtoto wa marehemu aitwaye Peter.
Hata hivyo James akulizika tena na kiwango hicho hivyo alitaka aongezewe pesa nyingine ndipo mwili wa marehemu uweze kuzikwa ndani ya kaburi .
Wakati wa majadiliano hayo yakiwa yanaendelea Padri Buyoyi ambae ni Paroko msaidi wa Parokia ya Maria Imakulata ilimlazimu asimamishe kwanza ibada kufuatia mabishano ya kundi na kabila la Waha na kikundi kidogo cha kabila la James.
Mtoto mkubwa wa marehemu aitwaye Baraka alimtaka James alipe shilingi elfu thelasini elfu inginezwa atafungwa na kamba ambazo na kuzikwa ndani ya kaburi pamoja na marehemu baba yake hata hivyo James akuwa anafedha kiasi hicho .
Baada ya kuwa ameshindwa kulipa fedha hizo kundi la vijana wa kabila la waha lilitaka kumkamata na aliweza kutimua mbio na hakufika mbali wakawa wamemkamata na kumrudisha katika eneo lililojirani na kaburi hilo kasha kuanza kumfunga kamba za naironi miguuni na mikononi licha ya kuomba wamsamehe lakini hawaku jari ombi lake .
Tukio hilo lilimlazimu Pdri Butoyi ashindwe kuendelea na ibada kwa zaidi ya dakta 20 baada ya hari kuwa yautulivu kasha aliendelea na ibada ya mazishi na mwili wa marehemu uliweza kuzikwa na muda wote huo James alikuwa ameendelea kufungwa kamba kwani alikuwa hana uwezo wa kuzifungua.
Baada ya mazishi kumalizika yaliochukua ndipo walipoamua kuanza kumfungua kamba miguuni na mikononi na ambapo kwa muda wote huo alikuwa amekaa kutoka na kutokuwa na uwezo wa kusimama.
Mwandishi wa gazeti hili ambae alikuwepo kwenye tukio hilo aliweza kufanya mahojiano na James ambae alisema hata fanya utani wa aina yoyote ila kwenye msiba na hata kwenye maeneo mengine .
Alisema mateso waliyompatia ni makubwa mno kwani mwili wake katika sehemu za miguu na mikono zimepata majeraha kutokana na kufungwa kamba kwa muda mrefu kwa kweli walionifanyia hivi hawana huruma alisema James.
0 comments:
Post a Comment