Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na George Mwigulu,Mpimbwe,Katavi.
Baadhi ya waumini wa dhehebu la Anglican Tanzania Dayosisi ya Ziwa Rukwa
wameaswa kupanda miti zaidi ya elfu tano kwa kila kanisa hilo lilipo
ili kuhuwisha juhudi za serikali za kuhifadhi na kutunza Mazingira.
Hayo aliyasema Jana Mchana Mchungaji kiongozi wa dhehebu hilo Joshua
Daniel Mugando wakati akiwahutubia Waumini kwenye hafra fupi za sherehe
ya ubatizo zilizofanyika kijiji cha Kashishi,kata ya Ikuba,Halmashauri
ya Mpimbwe,Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi.
Mch,Mugando alisema kuwa kanisa haliwezi kukubali kushuhudia Taifa kuwa
Jangwa kwa kuwavumilia baadhi ya watu wanaofanya uhalibifu wa kukata na
kuchoma misitu hovyo bali Kanisa kupitia Waumini wake linawapasa kuwa
Taa ya Jamii yote kwa kuwaelimisha hasara zitokanazo na uhalibifu wa
mazingira.
Aidha,Mchungaji Kiongozi huyo alibainisha kuwa uhalibifu wa mazingira
huchangia kwa asilimia kubwa mabadiliko ya hali ya hewa.Ambapo
husababisha mvua kutonyesha kwa muda muafaka ikiwa pamoja na kuhalibu
vyanzo vya maji ambapo mambo hayo ni hatari sana kwa maendeleo ya Taifa
lolote lile Duniani.
''Ndugu zangu Waumini,Ifahamike kuwa Kanisa linapaswa kuwa mfano Imara
katika kutunza mazingira kwa kupanda miche zaidi ya elfu tano kwa kila
Kanisa lilipo na ifikapo Mwaka 2020 Taifa letu Tanzania liwe lenye
kuvutia zaidi na kupafanya sehemu nzuri ya kuishi''Alisema Mch Mugando.
Sambamba na hayo Mch Mugando aliwataka waumini wote wa dhehebu la
Anglican Tanzania Dayosisi ya Ziwa Rukwa kupambana na mambo ya kimwili
kama vile kujiepusha kwa vijana juu ya matumizi ya madawa ya kulevya
ambapo yanaathali kubwa ya kudhohofisha nguvu kazi katika Taifa.
Nao baadhi ya waumini waliohudhuria katika hafra hiyo Jonas Rachael,Alex
Mwinamila na Mgdalena Paul walisema kuwa wako tayari kufanya kazi ya
Mungu kwa uadilifu mkubwa ikiwa pamoja na kuyatunza Mazingira hasa
katika wakati huu ambao Taifa linakabiliwa na uharibifu wa mazingira.
Home »
» WAUMINI WA DHEHEBU LA ANGILIKANA TANZANIA WAASWA KUTUNZA MAZINGIRA.
0 comments:
Post a Comment