Walter Mguluchuma
Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Genelali Mstaafu Raphael Muhuga ameziagiza Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi zenye maeneo yanayolima Tumbaku zitenge bajeti ya matengenezo ya barabara kwa ajiri maeneo yote yanayolima Tumbaku napia wajenge malambo ya maji kwa ajili ya mifugo ili kupunguza athari zinazo jitokeza za kugombea maji kati ya wakulima na wafugaji.
Agizo hilo alilitowa hapo jana wakati wa sherehe za uzinduzi wa msimu wa ununuzi wa masoko ya Tumbaku uliofanyika katika Kijiji cha Igagala chama cha Msingi cha ushirika wa Wakulima wa Tumbaku cha Mpanda Kati .
Alisema Serikali ya Mkoa inatambua kuwa zao la Tumbaku licha ya kuingiza kipato cha mkulima pia lina mchango mkubwa kwa Serikali kwa ujumla kwa ushuru unao tozwa kwa makampuni yanayonunua Tumbaku na upatikanaji wa fedha za kigeni kwa Tumbaku inayouzwa nje ya Nchi.
Mkuu huyo wa Mkoa alifafanua kuwa msimu wa kilimo wa 2014 na 2015 wakulima wa vyama vya ushirika wa Tumbaku vya Mkoa wa Katavi walizalisha kilo 11,910,459 ambazo ni sawa na Dola za Kimarekani 22,380,542 ambazo ni sawa na Tsh 44,761,085,440 ambapo Halmashauri za Mkoa wa Katavi zililipwa kiasi cha shilingi Bilioni mbili milioni mia mbili sitini na moja laki tisa na elfu tano kutokana na ushuru wa mauzo hayo ya Tumbaku .
Alitowa onyo kwa walanguzi wa Tumbaku na kwa wakulima wa Tumbaku wanauza pembejeo na Tumbaku kwa lengo la kukwepa madeni na kusababisha upungufu wa pesa za kuwalipa wakulima wanzao nakusababisha madeni yasiyo lipika au kulipwa.
Meja Jenarali mstaafu Muhuga alieleza kuwa bodi ya Tumbaku imepewa dhamana kubwa ya kuamua maslahi mapana ya wakulima hivyo wanao wajibu wa kuhakikisha mkulima anapewa bei halali kulingana na tumbaku ilivyo.
Na kwa makampuni yanayofanya hila za kudho0fisha harakati za wakulima wa Tumbaku kupitia vyama vyao vya ushirika katika kuondoa umaskini yatambue kwamba kufanya hivyo ni kosa kwani uchumi unaodidimizwa si wa mkulima peke yao bali ni wa Taifa pia hivyo Bodi ya Tumbaku Mkoani Katavi isimamie utekelezwaji wa Sheria na kanuni zinazoongoza kilimo cha Tumbaku Nchini Tanzania na si vinginavyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Tumbaku Mkoa wa Katavi LATCU Modesti Yamlinga aliziomba Halmashauri zilizopo katika Mkoa wa Katavi zitowe ushirikiano kwa vyama vya Ushiririka vya msingi katika suala la upadaji wa miti na wanaziomba zitenge bajeti kwa ajiri ya kufanikisha upandaji wa miti.
Yamlinga alisema wanaiomba Serikari isaidie vyama vya ushirika kapata zaidi makampuni ya ununuzi wa Tumbaku ili kuleta ushindani kwa makampuni yaliyopo ili vyama vya ushirika vipate uhuru wa biashara na kuongeza tija ya kipato na kuondoa adha kwa wakulima wao kwa usumbufu wanaosababishiwa na baadhi ya makampuni yaliyopo unao fanywa kwa makusudi.
Alieleza umefika wakati sasa kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi kuzifanyia ukarabati barabara za maeneo yanayolima Tumbaku ili magari yanayobeba kufika kwenye maghara ya kuuzia Tumbaku kwani lipo tatizo la magari kutofika kwa urahisi karibu kila eneo la chama cha Msingi kutokana na ubovu wa barabara .
Alisema chama Kikuu cha ushirika cha wakulima wa Tumbaku LATCU kinaundwa na vyama vya msingi saba ambavyo ni Nsimbo ,Katumba , Ilunde, Mishamo , Mpandakati ,Ukonongo na Kasokola na makampuni yanayonunua Tumbaku ni mawili tuu ambayo ni TLTC, Premium Active.
0 comments:
Post a Comment