Monday, June 6, 2016

WAUMINI WA DHEHEBU LA ANGILIKANA TANZANIA WAASWA KUTUNZA MAZINGIRA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


 Na George Mwigulu,Mpimbwe,Katavi.


Baadhi ya waumini wa dhehebu la Anglican Tanzania Dayosisi ya Ziwa Rukwa wameaswa kupanda miti zaidi ya elfu tano kwa kila kanisa hilo lilipo ili kuhuwisha juhudi za serikali za kuhifadhi na kutunza Mazingira.


Hayo aliyasema Jana Mchana Mchungaji kiongozi wa dhehebu hilo Joshua Daniel Mugando wakati akiwahutubia Waumini kwenye hafra fupi za sherehe ya ubatizo zilizofanyika kijiji cha Kashishi,kata ya Ikuba,Halmashauri ya Mpimbwe,Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi.


Mch,Mugando alisema kuwa kanisa haliwezi kukubali kushuhudia Taifa kuwa Jangwa kwa kuwavumilia baadhi ya watu wanaofanya uhalibifu wa kukata na kuchoma misitu hovyo bali Kanisa kupitia Waumini wake linawapasa kuwa Taa ya Jamii yote kwa kuwaelimisha hasara zitokanazo na uhalibifu wa mazingira.

Aidha,Mchungaji Kiongozi huyo alibainisha kuwa uhalibifu wa mazingira huchangia kwa asilimia kubwa mabadiliko ya hali ya hewa.Ambapo husababisha mvua kutonyesha kwa muda muafaka ikiwa pamoja na kuhalibu vyanzo vya maji ambapo mambo hayo ni hatari sana kwa maendeleo ya Taifa lolote lile Duniani.

''Ndugu zangu Waumini,Ifahamike kuwa Kanisa linapaswa kuwa mfano Imara katika kutunza mazingira kwa kupanda miche zaidi ya elfu tano kwa kila Kanisa lilipo na ifikapo Mwaka 2020 Taifa letu Tanzania liwe lenye kuvutia zaidi na kupafanya sehemu nzuri ya kuishi''Alisema Mch Mugando.

Sambamba na hayo Mch Mugando aliwataka waumini wote wa dhehebu la Anglican Tanzania Dayosisi ya Ziwa Rukwa kupambana na mambo ya kimwili kama vile kujiepusha kwa vijana juu ya matumizi ya madawa ya kulevya  ambapo yanaathali kubwa ya kudhohofisha nguvu kazi katika Taifa.


Nao baadhi ya waumini waliohudhuria katika hafra hiyo Jonas Rachael,Alex Mwinamila na Mgdalena Paul walisema kuwa wako tayari kufanya kazi ya Mungu kwa uadilifu mkubwa  ikiwa pamoja na kuyatunza Mazingira hasa katika wakati huu ambao Taifa linakabiliwa na uharibifu wa mazingira.

No comments:

Post a Comment