Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu blog
Baadhi ya Wanawake wa Kijiji cha Songambele Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wamejikuta katika wakati mgumu kutokana na kupokea vipigo na manyanyaso mengine kutoka kwa waume zao kutokana na kutumia muda mrefu katika kutafuta maji ambayo ni nitatizo kubwa sana Kijijini hapo .
Hayo yalisemwa hapo jana kwa uchungu mkubwa na baadhi ya Wanawake wa Kijiji hicho mbele ya Waandishi wa Habari waliokuwa wametembelea Kijiji hicho katika eneo la kisima cha kutekea maji kilichopo jirani na ofisi za Halmashauri ya Nsimbo.
Mmoja wa akinamama hao Maria Yohana alisema baadhi ya wanawake wa Kijiji hicho wamekuwa wakipgwa na waume zao kutoka na kuchelewa kupika chakula kunako sababishwa na foleni kubwa ya kuteka maji inayosababishwa na uhaba wa maji unaokikabili Kijiji hicho cha Songa Mbele .
Alisema wamekuwa wakilazimika kuamka usiku wa manane ili kuweza kuwahi foleni ya kuteka maji kwa ajiri ya matumizi mbalimbali ya nyumbani maji hasa ya kunywa kutoka na kijiji hicho kuwa kinategemea kisima kimoja tuu.
Zaluta Petro aliwaambia Waandishi wa Habari kuwa wamekuwa wakichukua zaidi ya saa tano kwa ajiri ya kupanga foleni hadi inapofika mtu zamu yake ya kuchota maji kutokana na kisima hicho kuwa na tatizo la kutotowa maji mengi na mara nyingine yamekuwa yakikatika .
Alisema wamekuwa wakipata shida sana kwa wame wao pindi wanakuwa wamechelewa kutoka kuchota maji hari ambayo imekuwa ikiwafanya wakati mwingine watuhumiwe na wame zao kuwa walikuwa kwa wanaume wengine kitu ambacho sio sahihi.
Kwa upande wake Cristina Sabuni alieleza kuwa amekuwa akichangazwa na Halmashauri ya Nsimbo kutotengeneza kisima hicho wakati wao wanapochota maji huwa wanalipia kiasi cha shilingi ishirini kwa kila ndoo moja .
Alifafanua kisima hicho pekeekijijini hapo kilijengwa mwaka 1995 kwa msaada wa aliyekuwa Mbunge wao ambae kwa sasa ni marehemu Monjor Sigela Nsima tungekuwa na uwezo wa kumfufua kungefanya hivyo alisema Cristina kwa masikitiko.
Nae Stephano Ally alieleza kuwa wameanza kufanya jitihada wao kama wakazi wa Kijiji hicho za kuchangishana fedha ili wachimbe kisima kitakacho wasaidia wake zao kuondokana na tatizo la maji.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Beatus Kambimbaya alisema wameisha iomba Halmashauri ya Nsimbo kukifanyia matengenezo kisima hicho ili maji yaweze kupatikana kwa wingi kwani ni muda mrefu sasa kisima hicho akijifanyiwa matengenezo .
Alisema ndio maana wakazi kijiji hicho wamekuwa wakiugua mara kwa mara baadhi ya magonjwa kutokana na baadhi yao kutumia maji ya kwenye madimbwi.
No comments:
Post a Comment