Tuesday, May 31, 2016

SHULE YA MH PINDA YAKOSA VYOO ZAIDI YA MIAKA MIWILI WANAFUNZI WAJISAIDIA VICHAKANI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



Na   Walter  Mguluchuma.
    Katavi

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya kata Usevya,Halmashauri ya Mpimbwe,Wilayani Mlele mkoani Katavi inakabiliwa na ukosefu wa matundu ya vyoo 35,Hali ambayo imewalazimu wanafunzi hao kujisaidia vichakani.


Wakizungumza na Waandishi wa Habari jana mchana shuleni hapa mbele ya Mkuu wa shule DenisThilia na Mwenyekiti wa bodi ya shule Kwilasa Machembe,Baadhi ya wanafunzi wanao soma kidato cha cha tano Juniour Mgallah na Moshi Rammadani walisema kukosekana kwa matundu ya vyoo katika shule yao imekuwa ikiwapa shida kutumia muda mwingi wa kutafuta sehemu ya kujisaidia.

''Inasikitisha sana,Shule pekee ya kidato cha tano na sita iliyo ndani ya eneo la Waziri mkuu mstahafu wa Tanzania Mh Piter Pinda kukosa matundu ya vyoo ya kukidhi mahitaji zaidi ya miaka miwili hadi matundu manne ya choo yaliyopo kujaa na kusababisha sasa tunajisaidia vichakani''Walisema.

Sanjali na hayo,Wanafunzi waliiomba Serikali na Wazazi wao kulishughurikia tatizo hilo la ukosefu wa vyoo kwa zaidi ya miaka miwili ambapo linaweza kuwahatarishia maisha pale patakapo weza kutokea mlipuko wa magonjwa hatari ya kipindupindu ikiwa pamoja na kuathiri mfumo wa kujifunza kwa kuwa mazingira kutOkuwa rafiki kwao.

Naye Mwenyekiti wa bodi ya  shule sekondari Usevya Kwilasa Machembe amekiri kukosekana vyoo kwa zaidi ya miaka miwili ambapo alisema kuwa hali hiyo imetokana na Serikali kufanya mbadiliko mara kwa mara ya Halmashauri ikiwa hapo awali walikuwa katika Halmashauri ya Mpanda,Mlele na hivi sasa Mpimbwe.Hivyo kusababisha baadhi ya miradi iliyokuwa imeibuliwa kukwama kumalizika na mingine kushindwa kutekekelezwa kila mabadiliko yanapo tokea.

Hata hivyo,Mkuu wa shule hiyo Denis Thilia alifafanua kuwa tatizo hilo ni mmoja ya mapungufu yaliyopo shuleni hapo ikiwa pamoja na upungufu wa mabweni matatu ya wanafunzi wa kike.Ambapo tayar ameshayatolea taarifa kwa mamulaka husika.

Kwa upande wa mkurungezi mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe Erasto Kiwale,Alisema taarifa hizo ameshazipokea na tayari amesha waagiza  watendaji wa kijiji na kata kulishughurika mara moja japo wanakabiliwa na ukata wa kifedha kutokana na Halmashauri hiyo kuwa mpya.

No comments:

Post a Comment