Katavi
Wakizungumza na Waandishi wa Habari jana mchana shuleni hapa mbele
ya Mkuu wa shule DenisThilia na Mwenyekiti wa bodi ya shule Kwilasa
Machembe,Baadhi ya wanafunzi wanao soma kidato cha cha tano Juniour
Mgallah na Moshi Rammadani walisema kukosekana kwa matundu ya vyoo
katika shule yao imekuwa ikiwapa shida kutumia muda mwingi wa kutafuta
sehemu ya kujisaidia.
''Inasikitisha sana,Shule pekee ya kidato cha tano na sita iliyo
ndani ya eneo la Waziri mkuu mstahafu wa Tanzania Mh Piter Pinda kukosa
matundu ya vyoo ya kukidhi mahitaji zaidi ya miaka miwili hadi matundu
manne ya choo yaliyopo kujaa na kusababisha sasa tunajisaidia
vichakani''Walisema.
Sanjali na hayo,Wanafunzi waliiomba Serikali na Wazazi wao
kulishughurikia tatizo hilo la ukosefu wa vyoo kwa zaidi ya miaka miwili
ambapo linaweza kuwahatarishia maisha pale patakapo weza kutokea
mlipuko wa magonjwa hatari ya kipindupindu ikiwa pamoja na kuathiri
mfumo wa kujifunza kwa kuwa mazingira kutOkuwa rafiki kwao.
Naye Mwenyekiti wa bodi ya shule sekondari Usevya Kwilasa
Machembe amekiri kukosekana vyoo kwa zaidi ya miaka miwili ambapo
alisema kuwa hali hiyo imetokana na Serikali kufanya mbadiliko mara kwa
mara ya Halmashauri ikiwa hapo awali walikuwa katika Halmashauri ya
Mpanda,Mlele na hivi sasa Mpimbwe.Hivyo kusababisha baadhi ya miradi
iliyokuwa imeibuliwa kukwama kumalizika na mingine kushindwa
kutekekelezwa kila mabadiliko yanapo tokea.
Hata hivyo,Mkuu wa shule hiyo Denis Thilia alifafanua kuwa tatizo
hilo ni mmoja ya mapungufu yaliyopo shuleni hapo ikiwa pamoja na
upungufu wa mabweni matatu ya wanafunzi wa kike.Ambapo tayar
ameshayatolea taarifa kwa mamulaka husika.
Kwa upande wa mkurungezi mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe Erasto
Kiwale,Alisema taarifa hizo ameshazipokea na tayari amesha waagiza
watendaji wa kijiji na kata kulishughurika mara moja japo wanakabiliwa
na ukata wa kifedha kutokana na Halmashauri hiyo kuwa mpya.
0 comments:
Post a Comment