MAKAMU Mkuu wa Shule ya Sekondari Usevya katika Halmashauri ya
Mpimbwe wilayani Mlele , Makonda Ng’oka “Membele” (34) amefikishwa
katika Mahakama ya mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi
wake.
Mshtakiwa huyo alifikishwa juzi mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama
hiyo, Chiganga Tengwa ambapo alikana shitaka lake na yupo nje baada ya
kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka kulipa kiasi cha Sh 3,000,000
mahakamani.
Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali, Gregory Mhangwa alidai
mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo katika shule ya
sekondari Usevya kati ya Novemba 2015 na Aprili 2016.
Alieleza mahakamani hapo kwamba katika kipindi hicho mshtakiwa
alimuingilia mwanafunzi wake huyo kinyume cha maumbile. Hakimu Tengwa
aliahirisha shauri hilo hadi Juni 26 , mwaka huu litakapotajwa tena.
Inadaiwa kuwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa Makamu Mkuu huyo
wa shule hiyo kunafuatia wanafunzi wa kiume wanaosoma Kidato cha Tano
katika shule hiyo kumkataa na kutishia kuandamana kupinga vitendo vyake
vya kuwalawiti wanafunzi wake.
Kufuatia msimamo wa wanafunzi hao iliwalazimu Ofisa Elimu mkoa wa
Katavi, Everest Hunji na Mkurugenzi Mtendaji Halmashari ya Mpimbwe
wilayani Mlele, Evaristo Kiwale kufika shuleni hapo Jumatatu jioni na
kuzungumza na wanafunzi hao.
Wanafunzi hao walidai kuwa mwalimu huyo amekuwa akiwalawiti baadhi
yao ikiwa ni adhabu mbadala wanapobainika kufanya makosa shuleni hapo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe, Kiwale
alisema vitendo vya ushoga havikubaliki na kwamba tayari hatua stahiki
zimeshachukuliwa za kumpeleka katika vyombo vya kisheria. “Msitaharuki
mnapomuona mwalimu huyo mitaani msidhani hajachukuliwa hatua yoyote
ile,” alisisitiza.
Chanzo Gazeti La Habari Leo
0 comments:
Post a Comment