Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu Blog
MAHAKAMA ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imeamuru ng’ombe wapatao 1,332 walio kamatwa toka kwa wafugaji wanne wakiwa wameingia ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi wataifishwe na kuwa mali ya Serikali huku wafugaji wenye mifugo hiyo wakihukumiwa kwenda jela miaka miwili.
Hukumu hiyo ya ilitolewa Mei 27 na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Odira Amworo baada ya mahakama kuridhika na ushahidi wa pande zote mbili ambapo upande wa mashtaka uliongozwa na Mwanasheria mwandamizi wa Serikali Mkoa wa Katavi Achiles Mulisi na upande wa utetezi uliongozwa na wakili wa kujitegemea Patrick Mwakyusa.
Katika kesi hizo mbili tofauti zilizotokea maeneo tofauti ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi ambapo kesi ya kwanza iliwahusisha mfugaji Ngusa Mtangi Mkazi wa Kijiji Ntazimbila na Charles Mtoka mkazi wa Kijiji cha Laela mkoani Rukwa.
Awali Mwanasheria Mwandamizi Mulisi alidai mahakamani hapo kuwa washitakiwa hao walikamatwa Aprili 23 mwaka huu wakiwa wamejenga na kuishi ndani ya Hifadhi ya Taifa huku wakiwa na Ng’ombe 780 ambao walikuwa wakichunga ndani ya Hifadhi katika eneo la Mto Kavuu.
Baada ya maelezo hayo washitakiwa walikana mashitaka waliosomewa na katika utetezi wao Mahakamani hapo walidai kuwa mifugo hiyo haikuwa ndani ya Hifadhi bali Askari wa TANAPA ndio waliwaswaga Ng’ombe hao na kuingiza ndani ya Hifadhi na kisha kuwakamata .
Hakimu Mkazi Amworo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo alisema kuwa Mahakama imewatia hatiani washtakiwa baada ya kupatikana na makosa mawili ikiwa ni kujenga na kuishi ndani ya Hifadhi na kosa la kuingiza mifugo na kufugia ndani ya Hifadhi ya Taifa .
Hivyo Mahakama imeamuru mifugo hiyo itaifishwe na iwe mali ya Serikali na washitakiwa wanahukumiwa kila mmoja kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya Tsh 500,000 ambapo walifanikiwa kulipa faini na kuepuka kwenda jela.
Katika kesi ya pili ambayo iliwahusu washitakiwa Shigela Mayunga(22) na Haruna Robart(12) wakazi wa Kijiji cha Ntalamila Wilayani Nkasi.
Washitakiwa hao walidaiwa kukamatwa na Ng’ombe 552 wakiwa wameingia nayo katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi na kuchungia wakati wakijua ni kinyume na sheria.
Hakimu Amworo akisoma hukumu hiyo aliiambia Mahakama kuwa washitakiwa wamepatika na hatia hivyo Mahakama imeamuru Ng’ombe wote 552 wataifishwe wawe mali ya serikali na washitakiwa watumikie jela kifungo cha miaka 2 kila mmoja au kulipa faini ya Tsh 700 ,000 kila mmoja.
Alieleza hata hivyo mshitakiwa wa pili Haruna Robart(12) Mahakama inamwachia huru kutokana na sheria ya watoto Namba tano ya mwaka 2009 ili awe na tabia njema na mshitakiwa wa kwanza alilipa faini na kuachiwa huru.

0 comments:
Post a Comment