Home » » SERIKALI IMEAMURU NG'OMBE 1,332 WALIOKAMATWA KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA KATAVI WATAIFISHWE NA KUWA MALI YA SERIKALI.

SERIKALI IMEAMURU NG'OMBE 1,332 WALIOKAMATWA KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA KATAVI WATAIFISHWE NA KUWA MALI YA SERIKALI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na Walter    Mguluchuma
Katavi yetu Blog

MAHAKAMA ya Wilaya  ya  Mpanda  Mkoani  Katavi  imeamuru ng’ombe wapatao  1,332   walio kamatwa  toka kwa wafugaji  wanne wakiwa wameingia  ndani  ya  Hifadhi ya  Taifa  ya  Katavi wataifishwe na kuwa  mali ya  Serikali  huku wafugaji wenye mifugo hiyo wakihukumiwa kwenda  jela miaka miwili.

Hukumu  hiyo ya  ilitolewa  Mei 27 na  Hakimu  Mkazi  wa   Mahakama hiyo  Odira  Amworo  baada ya mahakama kuridhika na  ushahidi wa  pande  zote  mbili  ambapo  upande wa mashtaka  uliongozwa  na  Mwanasheria   mwandamizi wa  Serikali  Mkoa wa  Katavi   Achiles  Mulisi  na  upande wa utetezi  uliongozwa  na wakili wa kujitegemea Patrick  Mwakyusa.

Katika  kesi   hizo  mbili  tofauti  zilizotokea  maeneo  tofauti ya  Hifadhi ya Taifa ya  Katavi   ambapo  kesi ya  kwanza iliwahusisha mfugaji Ngusa  Mtangi Mkazi wa  Kijiji  Ntazimbila  na  Charles  Mtoka  mkazi  wa  Kijiji  cha  Laela  mkoani Rukwa.

Awali Mwanasheria  Mwandamizi  Mulisi  alidai mahakamani hapo kuwa  washitakiwa  hao walikamatwa  Aprili  23  mwaka huu  wakiwa wamejenga na kuishi  ndani ya  Hifadhi ya Taifa  huku  wakiwa   na  Ng’ombe 780  ambao walikuwa wakichunga  ndani ya  Hifadhi  katika  eneo la Mto Kavuu.

Baada ya maelezo hayo washitakiwa  walikana  mashitaka waliosomewa  na  katika  utetezi wao  Mahakamani  hapo walidai kuwa  mifugo   hiyo  haikuwa   ndani ya  Hifadhi bali   Askari wa  TANAPA  ndio waliwaswaga    Ng’ombe  hao  na kuingiza  ndani ya  Hifadhi  na  kisha kuwakamata .

Hakimu  Mkazi  Amworo  baada ya kuridhika  na  ushahidi uliotolewa  Mahakamani  hapo  alisema kuwa Mahakama  imewatia  hatiani washtakiwa  baada ya kupatikana  na  makosa mawili  ikiwa ni kujenga na kuishi  ndani ya Hifadhi na  kosa la kuingiza mifugo na kufugia  ndani ya  Hifadhi ya Taifa .

Hivyo Mahakama  imeamuru   mifugo  hiyo itaifishwe  na  iwe mali ya  Serikali na washitakiwa  wanahukumiwa  kila  mmoja  kifungo cha miaka miwili jela au kulipa  faini ya  Tsh 500,000 ambapo  walifanikiwa  kulipa faini na kuepuka kwenda jela.

Katika  kesi ya  pili  ambayo iliwahusu washitakiwa  Shigela Mayunga(22) na Haruna Robart(12)  wakazi wa  Kijiji  cha  Ntalamila  Wilayani Nkasi.

 Washitakiwa hao walidaiwa  kukamatwa na Ng’ombe  552 wakiwa wameingia nayo katika  Hifadhi ya  Taifa ya  Katavi na  kuchungia  wakati wakijua ni kinyume na sheria.

Hakimu  Amworo  akisoma  hukumu  hiyo  aliiambia  Mahakama  kuwa washitakiwa wamepatika  na  hatia hivyo  Mahakama  imeamuru  Ng’ombe   wote  552 wataifishwe  wawe  mali ya  serikali   na washitakiwa watumikie  jela  kifungo cha miaka  2  kila  mmoja  au kulipa  faini ya  Tsh  700 ,000 kila  mmoja.

Alieleza  hata  hivyo  mshitakiwa wa pili   Haruna  Robart(12)  Mahakama  inamwachia  huru  kutokana  na  sheria ya watoto  Namba  tano ya mwaka  2009  ili  awe   na  tabia  njema na  mshitakiwa wa kwanza  alilipa  faini na kuachiwa  huru.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa