Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali mstaafu Raphael Muhuga amewaagiza Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote nne za Mkoa wa Katavi kuhakikisha fedha zote za Umma zilizolipwa kama msharaha hewa kwa watumishi 46 kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 200 zinarudishwa ndani ya siku 21.
Maagizo hayo aliyotowa hapo jana mbele ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa wa Katavi pamoja na Waandishi wa habari ofisini kwake wakati alipokuwa akitowa taarifa kuhusu idadi ya watumishi hewa waliobainika katika Mkoa wa Katavi .
Alisema Mkoa wa Katavi umebainika kuwa na Watumishi hewa 46 mpaka sasa ambao wameigharimu na kuitia hasara Serikali kiasi cha shilingi milioni 200,792,448.
Meja Jenerali Muhuga alifafanua kuwa Halmashauri ya Manspaa ya Mpanda katika taarifa za awali haikuwa na mtu mtumishi hewa hata mmoja wakati kwa sasa inawatumishi hewa 16 waliobainika na kuitia Serikali hasara ya Tsh 31,231,516 Halmashauri ya Nsimbo awali ilikuwa na watumishi hewa 17 kwa sasa wapo 11 ambao wameitia hasara Serikali kiasi cha Tsh 90,641,880 kutoka na watumishi kulipwa misharaha hewa.
Halmashauri ya Mlele awali katika zoezi la kuwabaini watumishi hewa walikuwa wawili kwa sasa wapo kumi walioigharimu Serikali kiasi cha Tsh milioni 45,650,900 na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda awali ilikuwa na watumishi wawili waliopo sasa ni tisa na wameigharimu Serikari na kuitia hasara kiasi cha Tsh Milioni 33,268,152.
Rc Muhuga alieleza kuwepo kwa watumishi hewa kumetokana na kuwepo kwa udhaifu na uzembe mkubwa wa Maafisa Utumishi wa Halmashauri ambao ndio wenye jukumu la kuwajibika kuhakikisha kuwa wanawafuta watumishi waliofikia ukomo katika mfumo wa taarifa za kiutumishi na misharaha LOWSON.
Mfumo huo unamilikiwa na kutumiwa na Maafisa Utumishi hivyo suala la uwepo wa watumishi hewa katika Halmashauri sio uzembe bali ni makusudi na lazima maafisa utumishi wawajibike.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kutokana na kubainika kuwepo kwa watumishi hewa katika Mkoa wa Katavi anaagiza Wakurugenzi wote wa Halmashauri za Mkoa wa Katavi wawajibike na kuhakikisha fedha zote za umma zilzolipwa kama misharaha hewa zinarudishwa ndani ya siku 21 na watowe taarifa na uthibitisho wa fedha hizo kurudishwa Serikalini.
Pia Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri hizo waakikishe wanawasimamia maafisa utumishi kuwafuta watumishi hewa wote waliobainika ndani ya siku saba kuanzia jana na hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa Maafisa Utumishi walihusika na swala hilo la watumishi hewa.
Meje Jenerali Muhuga alisema anaishukuru tume ya watu wane ilifanya kazi kubwa ya kuhakiki watumishi wote ana kwa ana katika Mkoa wa Katavi na ameitaka kamati hiyo iharakishe kukamilisha uchunguzi wa watumishi 15 ambao taarifa zao zina utata ili waweze kumpatia taarifa mapema na aweze kutowa maamuzi .
Na amewataka watumishi wa Umma Mkoani Katavi kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kufuata sheria , kanuni na taratibu za utumishi ,kwa wale watakao zembea au kujihusisha na uadilifu watawajibishwa na kuchukuliwa hatua kali kwa mijibu wa sheria .
0 comments:
Post a Comment