Na Walter Mguluchuma
Katavi
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Katavi imewapandini sha kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Mpandai Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Naomi Nko na godfrey Majuto mwandisi wa Manspaa ya Songea Chiyando Muyenjwa Matoke kwa tuhuma za matumizi mabaya ya nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri na kujipatia fedha kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 64.
Watuhumiwa hao walifikishwa jana kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa na kusomewa mashitaka na wanasheria wa TAKUKURU wa Mkoa wa Katavi Bahati Haule na Simon Buchwa .
Watuhumiwa hao ambao wote watatu walikuwa wakitetewa na mwanasheria Elias Kifunda wanadaiwa kutenda kosa hilo kinyume cha sheria cha kifungu cha 22 cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Wanasheria wa TAKUKURU walidai kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo hapo Januari 2 mwaka 2012 wakishirikiana na wakandarasi waliokuwa wakitengeneza barabara ya kutoka Nsemlwa ,Kasokola hadi Mtapenda na kutengeneza nyaraka za malipo ya kiasi cha shilingi milioni 64, 376,152
Washitaka hao wanadaiwa kutenda kosa hilo wakati wakiwa ni watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ambapo mshitakiwa wa kwanza Godfrey Majuto wakati huo alikuwa ni Mwandisi wa ujenzi na mshitakiwa wa pili Naomi Ndelilio Nnko alikuwa ni kaimu Mkugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ambapo kwa sasa ni mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na Majuto kwa sasa ni mwandisi wa Manspaa ya Songea.
Wanasheria hao wa kutoka TAKUKURU waliendelia kuiambia mahakama kuwa watuhumiwa hao watatu walishirikiana kutenda kosa hilo wakiwa na watuhumiwa wengine wawili ambao hawakuweza kufikishwa mahakamani hapo jana ambao waliwataja kuwa ni Petro Mwanoni na Beatus Bisesa ambao nao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote.
Baada ya kusomewa mashita hayo watuhumiwa wote watatu walikana mashitaka hayo na walipewa mashariti ya mdhamana ambapo kila mmoja alitakiwa kudhaminiwa kwa kiasi cha shilingi milioni kumi keshi hau mali ambayo haihamishiki na hati zao za kusafiria kuzikadhisha mahakamani
Hata hivyo watuhumiwa wawili Majuto na Nnko waliweza kutimiza masharti na kupewa mdhama ina mshitakiwa Chiyando Muyenjwa Matoke alishindwa kutimiza mashariki ya mdhamana na kupelekwa rumande.
Hakimu Mkazi mfawidhi Chiganga Ntengwa aliihairisha kesi hiyo hadi hapo Mei 28 mwaka huu kwa ajiri ya kupangiwa tarehe ya kuanza kusikilizwa
0 comments:
Post a Comment