Monday, May 9, 2016

RC ATOA AGIZO KWA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI KURUDISHA FEDHA ZOTE ZA WATUMISHI HEWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
  Katavi
Mkuu wa  Mkoa wa Katavi  Meja  Jenerali  mstaafu   Raphael  Muhuga  amewaagiza  Wakurugenzi  Watendaji wa  Halmashauri  zote    nne za  Mkoa wa  Katavi  kuhakikisha  fedha zote za Umma  zilizolipwa kama  msharaha  hewa  kwa watumishi  46 kiasi  cha  zaidi ya  shilingi  milioni 200 zinarudishwa   ndani ya siku 21.
Maagizo hayo  aliyotowa  hapo  jana  mbele ya  wajumbe wa  kamati ya ulinzi na  usalama wa  Mkoa wa  Katavi  pamoja  na  Waandishi wa  habari  ofisini  kwake   wakati alipokuwa  akitowa  taarifa kuhusu  idadi  ya  watumishi hewa  waliobainika   katika  Mkoa  wa  Katavi .
Alisema   Mkoa wa  Katavi  umebainika  kuwa  na  Watumishi  hewa   46  mpaka sasa  ambao  wameigharimu  na kuitia  hasara  Serikali  kiasi  cha  shilingi  milioni 200,792,448.
Meja  Jenerali  Muhuga  alifafanua kuwa   Halmashauri ya  Manspaa ya  Mpanda   katika  taarifa  za  awali  haikuwa  na  mtu mtumishi  hewa  hata  mmoja  wakati kwa  sasa inawatumishi  hewa  16 waliobainika  na kuitia  Serikali hasara ya  Tsh 31,231,516  Halmashauri ya   Nsimbo awali  ilikuwa  na  watumishi  hewa  17 kwa  sasa wapo  11 ambao wameitia  hasara  Serikali  kiasi  cha  Tsh  90,641,880 kutoka  na  watumishi kulipwa  misharaha  hewa.
  Halmashauri ya  Mlele  awali  katika  zoezi la kuwabaini watumishi  hewa  walikuwa  wawili  kwa   sasa wapo   kumi  walioigharimu  Serikali  kiasi cha  Tsh   milioni  45,650,900 na  Halmashauri ya  Wilaya ya  Mpanda  awali  ilikuwa na  watumishi  wawili waliopo sasa ni  tisa  na wameigharimu  Serikari na kuitia  hasara  kiasi  cha   Tsh Milioni    33,268,152.
Rc  Muhuga  alieleza  kuwepo kwa watumishi  hewa  kumetokana na kuwepo kwa  udhaifu  na  uzembe  mkubwa  wa  Maafisa   Utumishi   wa  Halmashauri   ambao  ndio  wenye  jukumu  la kuwajibika  kuhakikisha  kuwa wanawafuta watumishi  waliofikia  ukomo katika   mfumo wa taarifa za kiutumishi na misharaha  LOWSON.
Mfumo huo unamilikiwa  na kutumiwa  na Maafisa  Utumishi   hivyo  suala  la uwepo  wa  watumishi   hewa  katika  Halmashauri   sio  uzembe  bali ni makusudi na lazima  maafisa  utumishi  wawajibike.
Mkuu huyo wa  Mkoa  alisema  kutokana  na kubainika  kuwepo kwa watumishi  hewa  katika  Mkoa wa  Katavi   anaagiza  Wakurugenzi  wote wa  Halmashauri za  Mkoa wa  Katavi  wawajibike na  kuhakikisha  fedha  zote za umma  zilzolipwa  kama  misharaha  hewa  zinarudishwa   ndani ya  siku 21 na watowe  taarifa na uthibitisho wa  fedha  hizo  kurudishwa  Serikalini.
Pia  Wakurugenzi  Watendaji  wa  Halmashauri  hizo  waakikishe wanawasimamia  maafisa utumishi  kuwafuta  watumishi hewa  wote waliobainika   ndani ya  siku saba kuanzia  jana  na  hatua  za  kinidhamu  zichukuliwe kwa Maafisa  Utumishi  walihusika na swala hilo la watumishi  hewa.
Meje  Jenerali  Muhuga  alisema  anaishukuru  tume ya watu wane  ilifanya  kazi  kubwa ya kuhakiki watumishi  wote  ana kwa ana katika  Mkoa wa Katavi  na  ameitaka  kamati hiyo  iharakishe  kukamilisha  uchunguzi wa watumishi  15  ambao  taarifa zao  zina utata  ili waweze kumpatia taarifa mapema  na  aweze kutowa  maamuzi .
Na amewataka  watumishi  wa  Umma   Mkoani Katavi  kufanya kazi  kwa  uadilifu  mkubwa  na kufuata  sheria   , kanuni na  taratibu  za utumishi ,kwa wale  watakao zembea  au kujihusisha  na uadilifu  watawajibishwa  na kuchukuliwa  hatua kali  kwa mijibu wa sheria .

No comments:

Post a Comment