Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Shirika la Hifadhi la Wanyama pori Tanzania TANAPA Lipo kwenye utaratibu wa kubadili mfumo wa utendaji kazi kutoka mfumo wa awali wa kiraia na kuingia kwenye mfumo wa Kijeshi USU ilikukabiliana na hari ya sasa ya ujangili.
Hayo yalisemwa hapo jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasi na utalii Meja Generali Gaudensi Milanzi wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya miezi mitatu ya Askari 14 wa TANAPA wa ngazi mbambali katika chuo cha wanyama pori cha Mlele Mkoani Katavi .
Meja Generali Milanzi alisema mabadiliko hayo ya kimfumo ni matakwa ya sheria ya uhifadhi wa wanyama pori Na 5 ya mwaka 2009 kifungu namba 10,11, 12 na 13 ambayo imeanisha wazi kwamba ili kuhakikisha ulinzi kamili wa maliasili katika maeneo yaliyohifadhiwa ,kutaundwa kikosi cha jeshi USU(pa
Aileleza kuwa Askari wa TANAPA wamekuwa wakuwa wakifanya kazi kiraia wakati majangili walioko kwenye hifadhi za Taifa na kwenye mapori ya akiba wanatumia silaha za kivita hari ambayo imekuwa ikipelekea ugumu wa kiutendaji wa kazi .
Aidha ni imani yake kuwa kupitia mafunzo walioyapata askari hao wamejifunza mengi yanayohusiana na dhana nzima ya uongozi na nidhamu haswa katika kipindi hiki ambacho uhifadhi unashuhudia mmomonyoko mkubwa wa maaadili kwa watumishi ,ujangili wenye kutumia mbinu za kisasa mfano tukio la hivi karibuni la majangili kuipiga na kuidondosha helikopita iliyokuwa inafanya doria katika pori la maswa ambao ulihusisha watumishi wa sekta ya uhifadhi.
Alisema Taifa kwa kipindi cha hivi karibuni ilmeshuhudia mmomonyoko mkubwa sana wa maadili kwa watumishi wake haswa wa ngazi ya askari hivyo aliwaomba wahitimu hao wawe kioo na kielelezo kizuri cha uhifadhi katika vituo vya kazi .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Genarali Mstaafu Raphael Muhuga alisema wale wote ambao walikuwa wanajihusisha na ujangili na kuingiza mifugo yao katika hifadhi ya Taifa ya Katavi watambue kuwa wakati wao kwa sasa umekwisha .
Alisema viongozi wa siasa wamekuwa wakiingilia mara kwa mara zoezi la operesheni la kuhamisha watu wanao vamia maeneo ya hifadhi kwa kisingizio cha kuwazingizia askari wanaofanya zoezi la kuwahamisha wavamizi kuwa kuwa wakati wanapokuwa wanafanya zoezi hilo huwa wanabaka yeye kama Mkuu wa Mkoa hatakuwa tayari kuona mali asili zinahujumiwa katika Mkoa wake .
Na ataendelea kushirikiana na TANAPA kuhakikisha mifugo yote ambayo imeingia kwenye hifadhi inaondolewa na amewaagiza viongozi wa serikali za vijiji kutenga maeneo ya matumizi bora ya ardhi.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa shirika la TANAPA Alan Kijazi alisema TANAPA imejipanga kuhakikisha inatowa mafunzo mbalimbali kwa askari wake ili kuweza kukabiliana na swala zima la ujangili hapa Nchini.
Alisema mafunzo hayo waliopata wahitimu hao ni muhimu sana kwa askari wa TANAPA na yanatokana na kukabiliana na hari kubwa ya ujangili ambao sasa hivi umechukua sura nyingine kutokana na majangili kuanza kutumia silaha za kisasa zaidi .
Aliiomba Wizara ya Mali Asili na utalii izifanyie kazi changamoto zote za shirika la TANAPA ililiweze kufanya kazi zake za kwa ufanisi mkubwa na kuendelea kulinda rasilimali za nchi yetu .
Alisema mafunzo katika chuo hicho yatakuwa ni endelevu kwani wanatarajia kufanya mafunzo mengine hivi karibuni kwa ajiri ya mameneja wa makao makuu na wahifadhi wakuu ambao jumla yao 21 ilikuimarisha mfumo huo wa jeshi Usu na baada ya mafunzo hayo kwa viongozi kumalizika wataanza mafunzo kwa askari wote wa TANAPA.
Kaimu Meneja wa mapori ya akiba ya Rukwa Lwafi Mark Chuwa alisema kuwa Idara ya wanyama pori na hifadhi za Taifa waliisha kukubaliana kushirikiana kukuza utalii hapa nchini .
Msoma risala ya wahitimu hao Stela Mwangoka alieleza kuwa mafunzo hayo ni mojawapo ya hatua muhimu ya shirika la hifadhi za Taifa Tanzania kutekeleza muundo mpya wa kurugenzi ya uhifadhi wa kuingia katika mfumo wa jeshi Usu ambao kwa sasa unatumika kwenye Taasisi nyingi za kiuhifadhi katika Bara la Afrika na pia katika kutekeleza sheria elekezi kwa Taasisi za uhifadhi wanyama pori Tanzania.
Alisema mafunzo hayo yaliwashirikisha pia wahifadhi mbalimbali na makao makuu ya shirika katika mafunzo hayo ya awamu ya tano Wahifadhi 26 ni wahifadhi wafawidhi,wahifadhi wandamizi na wahifadhi wasaidizi na askari wa ajira mpya wa TANAPA
No comments:
Post a Comment