Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi akionesha Meno ya Tembo aliyokutwa nayo Mchungaji wa Kanisa la Moraviani Katavi- Picha na Katavi yetu
Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu Blog
MCHUNGAJI wa kanisa la Moraviani Usevya Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi Gondwe Siame amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda na kusomewa mashitaka ya tuhuma ya kukamatwa na meno ya Tembo 11 yenye thamani ya shilingi milioni 90 akiwa ameyahifadhi ndani ya Kanisa analo liongoza.
.
Mtuhumiwa alipandishwa kizimbani hapo juzi majira ya saa 3;30 mbele ya hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo Chiganga Ntengwa na kusomewa mashtaka na
mwanasheria wa wa serikali Mkoa wa Katavi Jamila Mzirai..
Mbele ya mahakama hiyo mwanasheria huyo alidai kuwa mnamo siku ya Mei
5 majira ya saa saba mchana mtuhumiwa alikamatwa na polisi pamoja na Askari wa TANAPA wa Hifadhi ya Katavi akiwa na meno ya tembo 11 yenye thamani ya Tsh Milioni 90 akiwa ameyahifadhi ndani ya Kanisa la Moroviani Usevya. kinyume cha sheria .

Mtuhumiwa baada ya kusomewa mashitaka
hayo hakutakiwa kujibu lolote juu ya shitaka linalomkabili kwa kuwa
Mahakama hiyo ya Wilaya haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya
kuhujumu uchumi inayozidi kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 10. mpaka
iwe imepatiwa kibali.
Wakiri wa mtuhumiwa Patrick Mwakyusa
aliiomba na kuitaka Jamhuri kuleta kibali cha kuiruhusu Mahakama
hiyo kuendelea kuisikiza kesi hiyo ..
Mwanasheria huyo alidai kuwa mshitakiwa ni haki yake kupatatiwa mdhamana kwa kuwa kosa hilo linarusu mdhamana .
Hata hivyo mtuhumiwa Mchungaji
Gondwe Siame alipelekwa Mahabusu baada ya hoja zake hizo
kutoweza kukubalika Mahakamani hapo .
Hakimu Mkazi Mfawidhi Chiganga
Ntengwa aliharisha kesi hiyo hadi hapo Mei 23 itakapo tajwa
tena katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda.
0 comments:
Post a Comment