Home » » CHAMA CHA WAALIMU CWT WILAYA YA MPANDA CHATOWA MSAADA WA MADAWATI

CHAMA CHA WAALIMU CWT WILAYA YA MPANDA CHATOWA MSAADA WA MADAWATI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

  Na  Walter  Mguluchuma 
    Katavi
  Chama  cha  Waalimu  CWT  Wilaya ya Mpanda kimetowa msaada wa Madawati yenye thamani ya zaidi ya  shilingi milioni 1.3 kwa  shule ya Msingi  Mnyagala  Halmashauri ya  Wilaya ya Mpanda  inayokabiliwa na tatizo la ukosefu wa madawati hari ambayo inawafanya Wanafunzi 732 wasome huku wakiwa wamekaa chini .
Msaada huo wa  Madawati 20 uliotolewa  Chama hicho cha Waalimu ulikabidhiwa  hapo  jana  na  Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya  Mpanda   Jumanne  Msomba  kwa  Mwalimu  Mkuu wa  shule ya Msingi  Mnyagala  Sikazwe  Jafhet   makabidhiano hayo yalifanyika  katika  shule hiyo na kushuhudiwa na  Waalimu na  Wanafunzi wa shule  hiyo .
Mwenyekiti  huyo wa  Chama  cha  Waalimu  alisema  chama  hicho kimetowa  msaada  huo wa  madawati 20  yenye  thamani ya  Tsh 1 ,470,000 baada ya kuwa wamepata  taarifa ya  upungufu  mkubwa wa  madawati unao  ikabili  shule  hiyo ya  Msingi .
Msomba  alieleza  kitendo cha mwanafunzi kusoma  shule  huku  akiwa amekaa chini kunasababisha wanafunzi kutoipenda shule na  matokeo yake ni kuwa mtoro   wa  shele.
 Pia  alitowa  wito kwa wadau  mbalimbali katika  Wilaya ya  Mpanda  kuwa na utaratibu wa kutowa msaada katika  sekta ya  Elimu kwani michango ya wananchi  inahitajika  sana  katika kuendeleza elimu
  Awali  kabla ya kukabidhiwa  madawati  hayo   Mwalimu  Mkuu wa  shule  hiyo ya Msingi  Mwamkulu    Sikazwe  Japhet alieleza  kuwa  shule  hiyo  yenye   jumla ya  wanafunzi  1150  ina   vyumba   vinne vya   madarasa  hivyo  inakabiliwa  na  tatizo  kubwa la  upungufu  madawati  hari  ambayo  inawalazimu  wanafunzi  732 kusoma  huku wakiwa wamekaa chini.
  Alieleza   shule  hiyo  inaidadi ya  madawati  119  wakati  mahitaji  yao ni  madawati  244  hivyo  msaada  huo waliopata  utasaidia kupunguza  tatizo la  wanafunzi  kukaa  chini kwahidadi ya madawati  hayo  20 waliopewa na CWT yatatumiwa  na  wanafunzi 60.
 Aliitaja  changamoto  nyingine inayoikabili  shule   kuwa ni uhaba  wa  majengo ya  madarasa   kwani  shule  hiyo inavyumba  vinne  tuu vya  madarasa   wakati  mahitaji yao ni   vyumba  22  hari ambayo  huwalazimu  waalimu kusimamisha  masomo wakati wa  mvua  na kuwakusanya  wanafunzi   kwenye   vyumba   vya  madarasa  hadi hapo  mvua  inapokuwa imekatika .
Kwa  upande  wake  mwanafunzi wa  darasa  la  saba  Jackson  Raban  alieleza  kuwa    ni  ukweli  usiopingika  shule   yao  inakabiliwa  na  tatizo la  upungufu wa  madawati  hari  ambayo  inawafanya  wao wanafunzi wa  darasa  la  saba kukaa kwenye  dawati  moja  wanafunzi wane  badala ya wanafunzi wawili  huku  wengi wa wanafunzi wa  madarasa ya chini wakiwa wanasoma wakiwa wamekaa chini na baadhi ya  madarasa wakiwa wanasomea  nje  chini ya miti.
Mjumbe wa  kamati  tendaji ya  CWT  Wilaya  ya  Mpanda   Richald  Chitambala  aliwataka  waalimu  wale  ambao hawajajiunga  na  chama   cha  waalimu waone  umuhimu wa kuwa  wanachama . 
 Alisema  miongoni  mwa   kazi za  chama  cha  Waalimu   kinazo  zifanya ni  kuwatetea waalimu  katika  kudai  masilahi yao  mbalimbali .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa