Na Walter Mguluchuma
Katavi
Chama cha Waalimu CWT Wilaya ya Mpanda kimetowa msaada wa Madawati yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 1.3 kwa shule ya Msingi Mnyagala Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda inayokabiliwa na tatizo la ukosefu wa madawati hari ambayo inawafanya Wanafunzi 732 wasome huku wakiwa wamekaa chini .
Msaada huo wa Madawati 20 uliotolewa Chama hicho cha Waalimu ulikabidhiwa hapo jana na Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Mpanda Jumanne Msomba kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mnyagala Sikazwe Jafhet makabidhiano hayo yalifanyika katika shule hiyo na kushuhudiwa na Waalimu na Wanafunzi wa shule hiyo .
Mwenyekiti huyo wa Chama cha Waalimu alisema chama hicho kimetowa msaada huo wa madawati 20 yenye thamani ya Tsh 1 ,470,000 baada ya kuwa wamepata taarifa ya upungufu mkubwa wa madawati unao ikabili shule hiyo ya Msingi .
Msomba alieleza kitendo cha mwanafunzi kusoma shule huku akiwa amekaa chini kunasababisha wanafunzi kutoipenda shule na matokeo yake ni kuwa mtoro wa shele.
Pia alitowa wito kwa wadau mbalimbali katika Wilaya ya Mpanda kuwa na utaratibu wa kutowa msaada katika sekta ya Elimu kwani michango ya wananchi inahitajika sana katika kuendeleza elimu
Awali kabla ya kukabidhiwa madawati hayo Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya Msingi Mwamkulu Sikazwe Japhet alieleza kuwa shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 1150 ina vyumba vinne vya madarasa hivyo inakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu madawati hari ambayo inawalazimu wanafunzi 732 kusoma huku wakiwa wamekaa chini.
Alieleza shule hiyo inaidadi ya madawati 119 wakati mahitaji yao ni madawati 244 hivyo msaada huo waliopata utasaidia kupunguza tatizo la wanafunzi kukaa chini kwahidadi ya madawati hayo 20 waliopewa na CWT yatatumiwa na wanafunzi 60.
Aliitaja changamoto nyingine inayoikabili shule kuwa ni uhaba wa majengo ya madarasa kwani shule hiyo inavyumba vinne tuu vya madarasa wakati mahitaji yao ni vyumba 22 hari ambayo huwalazimu waalimu kusimamisha masomo wakati wa mvua na kuwakusanya wanafunzi kwenye vyumba vya madarasa hadi hapo mvua inapokuwa imekatika .
Kwa upande wake mwanafunzi wa darasa la saba Jackson Raban alieleza kuwa ni ukweli usiopingika shule yao inakabiliwa na tatizo la upungufu wa madawati hari ambayo inawafanya wao wanafunzi wa darasa la saba kukaa kwenye dawati moja wanafunzi wane badala ya wanafunzi wawili huku wengi wa wanafunzi wa madarasa ya chini wakiwa wanasoma wakiwa wamekaa chini na baadhi ya madarasa wakiwa wanasomea nje chini ya miti.
Mjumbe wa kamati tendaji ya CWT Wilaya ya Mpanda Richald Chitambala aliwataka waalimu wale ambao hawajajiunga na chama cha waalimu waone umuhimu wa kuwa wanachama .
Alisema miongoni mwa kazi za chama cha Waalimu kinazo zifanya ni kuwatetea waalimu katika kudai masilahi yao mbalimbali .
No comments:
Post a Comment