Na Walter Mguluchuma
Katavi
Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na har akati za kupunguza umaskini ,Maafa na kutunza mazingira katika Mikoa yote ya Tanzania Bar limepanga kuanzisha Benki ya wajasilia mali ya waandesha pikipiki BODA BODA hapa Nchini ili kuweza kuwakomboa Boda Boda kiuchumi.
Kauli hiyo ilitolewa hapo juzi na Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa APEC Respicius Timanywa kwa nyakati tofauti wakati wakati wa kufunga mafunzo ya watumiaji vvyombo vya moto barabarani katika ukumbi wa Galden Mjini Mpanda na katika ukumbi wa Mnyaki makazi ya wakimbizi ya Katumba.
Mafunzo hayo ya watumiaji wa vyombo vya moto yalifanyika katika vituo viwili vya Mpanda Mjini na Mnyaki Katumba yaliotumia siku saba yaliwashirikisha washiriki 220 ambapo wahimu wa mafunzo hayo walikabidhi vyeti vya uhitimu na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Salimu Shilingi ambae ni Katibu Tawala na utumishi wa Mkoa wa Katavi .
Alisema Taasisi hiyo itaandaa mkutano hivi karibuni Mjini Dodoma utakao washirikisha viongozi wa Bodaboda wa kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara ili kujadiliana na kuwepa mipango ya uanzishwaji wa Banki ya Wajasiliamali wa Boda boda hapa Nchini kwa lengo la kuwakomboa kiuchumi.
Alisema Banki hiyo itakapoanzishwa itakuwa ni mkombozi kwao kwani itaweza kuwasaidia kuinua kipato chao kwa kupitia vikundi watakavyo kuwa wameviunda na kupata mkopo kupitia Banki hiyo.
Timanya alisema APEC inaendelea na mkakati wa kutowa mafunzo kwa waendesha pikipiki wa mikoa yote kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ambapo wamefanikiwa kufika na kutowa mafunzo karika Tarafa zote za Mikoa ya Dares salaam, Tanga , Morogoro , Shinyanga ,Simiyu, Ruvuma na Mbeya.
Aliitaja Mikoa mingine kuwa ni Njombe,Manyara, Arusha , Singida , Geita Dodoma , Tabora Pwani , Mtwara , Kilimanjaro Rukwa na Iringa na jumla ya watumiaji wa zaidi ya laki mbili wa vyombo vya moto barabarani wameisha patiwa mafunzo .
Pia aliliomba jeshi la polisi upande wa usalama barabarani kufanya kazi kwa uadilifu na kwa kuzingatia maadali ya kazi zao kwani kunawakati watumiaji wa vyombo vya moto wamekuwa wakiwaona wao ni maadui kutoka na kutozingatia maadili ya kazi na madreva nao wanapaswa kutii na kufuata sheria za barabarani
Kwa upande Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenelali Raphael Muhuga katika hutuba yake ya kufunga mafunzo hayo iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala na utumishi wa Mkoa wa Katavi Salumu Shilingi alisema umefika wakati sasa wa mtu yoyote ambae hajapatia kwenye mafunzo kama hayo asipatiwe leseni.
Alisema watu wamekuwa wakikimbilia kukata leseni bila kuwa wamepitia kwenye mafunzo na ndio wamekuwa chanzo cha kusababisha ajari nyingi hapa Nchini .
Nashauri leseni zisitolewe kwa mtu yoyo ambae haja patiwa mafunzo kama hayo hivyo waliohitimu wanao wajibu wakuhamasisha ambao hawajapata mafunzo nao kufanya hivyo .
Mwenyekiti wa Bodaboda wa Mkoa wa Katavi alisema hayuko tayari kuona mtu anae vunjwa sheria za usalama barabarani alafu anakimbilia kwake kuomba msaada wa kumtetea.
Aliomba mtambo wa kutolea leseni za unidereva Mkoa Katavi uwekwe ilikuwapunguzia adhaa za kwenda kukatia Leseni Mkoani Rukwa na hari ambayo imekuwa ikiwafanya baadhi ya Boda boda kushindwa kukata leseni kutoka na ghama ya kublanzi .
Mmmoja wa washiriki na mhitimu wa mfunzo hayo Afred Kpeta alilishukuru shirika la Apec kwa kutowa mafunzo hayo nakuliomba shirika hilo kurudi tena mkoa hapa na kutowa mafunzo kwa mara nyingine tena kwani mafunzo kama hayo bado yanahitajika sana Mkoani Katavi
No comments:
Post a Comment