Thursday, May 19, 2016

HOT NEWS: MCHUNGAJI ALIYEKAMATWA NA MENO YA TEMBO AKIWA AMEYAHIFADHI KANISANI AFIKISHWA KIZIMBANI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi akionesha Meno ya Tembo aliyokutwa nayo Mchungaji wa Kanisa la Moraviani Katavi- Picha na Katavi yetu
Na  Walter  Mguluchuma
Katavi yetu Blog

MCHUNGAJI wa kanisa la Moraviani Usevya  Tarafa  ya  Mpimbwe  Wilaya ya  Mlele  Mkoa  wa  Katavi Gondwe  Siame  amepandishwa kizimbani katika  Mahakama ya  Wilaya ya  Mpanda na kusomewa mashitaka ya tuhuma ya kukamatwa na  meno ya  Tembo 11 yenye  thamani ya  shilingi milioni  90 akiwa ameyahifadhi ndani ya Kanisa analo liongoza.
.

   Mtuhumiwa alipandishwa kizimbani  hapo juzi  majira ya saa 3;30 mbele ya hakimu  Mkazi   Mfawidhi   wa mahakama hiyo Chiganga Ntengwa na kusomewa mashtaka na
mwanasheria wa wa serikali Mkoa wa  Katavi Jamila Mzirai..

Mbele ya mahakama hiyo mwanasheria huyo alidai   kuwa mnamo siku ya Mei
  5  majira ya saa  saba  mchana  mtuhumiwa  alikamatwa  na polisi pamoja  na  Askari wa   TANAPA  wa  Hifadhi ya  Katavi akiwa  na  meno ya  tembo 11  yenye  thamani ya  Tsh  Milioni  90  akiwa   ameyahifadhi  ndani ya  Kanisa la  Moroviani   Usevya. kinyume  cha  sheria .

 Mtuhumiwa  baada  ya  kusomewa  mashitaka  hayo  hakutakiwa kujibu lolote  juu ya shitaka  linalomkabili  kwa kuwa  Mahakama  hiyo ya  Wilaya haina  mamlaka  ya kusikiliza  kesi ya kuhujumu  uchumi inayozidi kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 10. mpaka iwe imepatiwa kibali.
Wakiri wa  mtuhumiwa   Patrick  Mwakyusa  aliiomba  na kuitaka  Jamhuri   kuleta kibali  cha kuiruhusu  Mahakama  hiyo  kuendelea kuisikiza  kesi hiyo ..
 Mwanasheria  huyo  alidai  kuwa   mshitakiwa ni haki yake kupatatiwa  mdhamana  kwa kuwa kosa hilo linarusu mdhamana .
 
  Hata  hivyo  mtuhumiwa  Mchungaji   Gondwe   Siame  alipelekwa     Mahabusu  baada ya  hoja  zake  hizo  kutoweza kukubalika   Mahakamani   hapo .
Hakimu   Mkazi    Mfawidhi   Chiganga   Ntengwa  aliharisha  kesi  hiyo  hadi  hapo  Mei  23  itakapo  tajwa  tena  katika  Mahakama ya  Wilaya ya  Mpanda.

No comments:

Post a Comment