N a Walter Mguluchuma
Katavi yetu blog
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima amewataka akinadada POA wanauza miili yao katika Mitaa mbalimbali ya Manspaa ya Mpanda kuacha tabia ya kuuza miili yao wafike ofisini kwake ili awapatie wataalamu wa kuwaelimisha kuunda vikundi vitakavyo wawezesha kujiinua kiuchumi badala ya kuuza mili yao .
Kauli hiyo ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda ameitowa ikiwa ni siku chache baada ya kuwa ameliagiza jeshi la Polisi Wilayani Mpanda kufanya msako wa kuwakamata na kuwaondosha akina dada POA wote wanaofanya biashara ya kuuza miili yao katika Mitaa ya Mji wa Mpanda .
Mwamlima aliwaambia waandishi wa Habari juzi kuwa mbali ya agizo hilo ameliagiza jeshi hilo kufanya ukaguzi wa kuzibaini nyumba zote Bubu za kulala wageni na na zitakazobaini wazifunge mara moja kwani ndio ambazo zimekuwa zikitumiwa na akina Dada POA kufanyia biashara ya kuuza mili yao.
Aliitaja mitaa ambayo hasa inatakiwa zoezi hilo lifanyike kuwa ni M itaa ya Simba , Fisi na Mtaa wa Majengo ambayo ndio inayoongoza kwa biashara ya Dada poa .
Alisema kuliko wao akina Dada wanao uza miili yao kuendelea kukamatwa kamatwa waambieni waje ofisini ili awapatie wataalamu watakao waelekeza namna ya kuunda vikundi vitakavyo wasaidia kukopesheka na kuweza kuwainua kiuchumi na kuwafanya wajitegemee.
Hivi karibuni biashara ya akina Dada wanaouza miili yao imeshamili sana katika Mji wa Mpanda baada ya kuvamiwa na akina dada poa ambao wengi wao wametoka katika Mikoa ya Mwanza Shinyanga , Mbeya na Kigoma.
Na wamekuwa wakimiliki nyumba mbili za kulala wageni katika Mta a wa Majengo B baada ya kudai kuwa kwenye madanguro wamekuwa wakisuburiwa kwa kukamatwa mara kwa mara tofauti na walivyo hamia kwenye Geusti hizo wamekuwa awasumbuliwi kwa kuwa wanachangia kodi ya Serikali kutokana na malipo wanayo mlipa mwenye Geusti alisema Dada Poa aliyejitambulisha kwa jina la Eliza mwenyeji wa Mwanza alipokuwa akionge na gazeti hili katika Mtaa wa Fisi.
Alisema wateja wao wanaowapa kwa wingi ni vijana mwenye umri unaoanzia miaka 16 na baadhi yao ni wanafunzi wavulana wa shule za Sekondari na biashara hiyo ya kuuza miili yao huwa wanaanzia shilingi 2,000 na kwasiku moja huwa wanapata kiasi kisichopungua shilingi 15,000 kwa siku .
Mmoja wa wakazi anae ishi kwenye mtaa huo Osca Selemani alieleza kuwa foleni ya wanaume wanaowafuata akina dada Poa huwa inaanza kuanzia saa moja na nusu jioni hadi saa sita usiku ndipo wakundi hayo ya wanaume yanapopungua .
Alisema yeye binafsi anajuta kujenga nyumba na kuishi kwenye mtaa huo kutokana na mtaa huo kuonekana kuwa hauna heshima kwenye jamii hali ambayo inamfanya ikifikia mida ya jioni kwenda yeye mwenyewe kutafuta mahitaji dukani kwa kuhofia mke wake na mtoto wake wa kike nao pia wanaweza wakadhaniwa ni Dada POA.
No comments:
Post a Comment