Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu blog
Chama cha Waalimu CWT Wilaya ya Mpanda kimetowa mafunzo kwa waalimu Viongozi Wanawake katika sehemu ya kazi mafunzo yakuwafanya Waalimu Wanawake wafahamu haki zao na kuzilinda na ujasiliamali
Mafunzo hayo ya siku moja yalifanyika jana katika ukumbi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda na kufunguliwa na Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Mpanda Jumanne Msomba.
Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo hayo Msomba alieleza kuwa Waalimu Wanawake wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalilmali ambazo wamekuwa wakishindwa kuzipatia ufumbuzi kutokana na kutofahamu haki zao zinazo walinda.
Alisema ndio maana CWT kitengo cha Wanawake imeona umuhimu wa kuwapatia mafunzo hayo ya siku moja yenye lengo la kuwafundisha watambue haki zao na sheria za utumishi pamoja na ujasilmali ili waweze kujiongezea kipato chao .
Mwenyekiti huyo aliwataka Waalimu kufanya kazi kwa kufuata taratibu za kazi katika utumishi wao kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa kujituma iliweweze kutekeleza vizuri majukumu ya kazi yao za kila siku .
Pia wawe karibu na chama chao cha Waalimu na wawe ushirikiano na pindi mwalimu mwanamke anapokuwa amepata matatizo sehemu ya kazi apelike mapema taarifa CWT .
Nae Kaimu Katibu wa CWT Wilaya ya Mpanda Masanja Manyanga alisema Kitengo cha wanawake cha CWT kinalojukumu la kuwakumbusha walimu wanawake majukumu yao .
PIa aliwataka waalimu wa Wanawake waweze kujitambua kwa kuvaa mavazi yenye heshima na wewe na lugha nzuri kwa jamii inayowazunguka pamoja na kuwa na tabia ya kuwashauri wanafunzi wa kike pindi wanapoona mwenendo wao unapokuwa umeanza kubadilika kimaadili .
Manyanga alisema chama cha Waalimu kimeamua kuwapatia mafunzo waalimu wanawake ya ujasiliamali ili waweze kujitambua na waweze kujipatia kipata kitakachowafanya watoke kwenye uchumi dhaifu .
Alisema bado baadhi ya watu wanazoimani potofu wanaamini kuwa mwanamke hastahili kumiliki mali yoyote jambo ambalo sio sahihi .
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Mwalimu Siyawezi Machulo alisema wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali wao kama waalimu .
Alitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni kutolipwa fedha za likizo kwa kipindi cha muda mrefu sasa na kutorekebishiwa mishahara kwa wakati pindi wanapokuwa wamepandishwa daraja .
No comments:
Post a Comment