Saturday, May 28, 2016

WALIMU WANAWAKE WAMEIOMBA SERIKALI KUHESHIMU SHERIA YA NDOA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



Na  Walter  Mguluchuma
    Katavi yetu blog

 Walimu  Wanawake   Wilayani  Mpanda  Mkoa  wa  Katavi  wameiomba   Serikali  kuheshimu   sheria ya   ndoa  ambayo inaruhusu  mtumishi  anapofunga  ndoa kumfuata     mwezi wake  ili waishi pamoja   kutokana  na waajiri  kuipuuza  na kuwanyima  uhamisho  hivyo  kumechangia  ndoa  nyingi kuvunjika .
 Maombi  hayo ya  walimu wa Wanawake kwa  Serikali yalitolewa  hapo  jana  na   Walimu  Viongozi wanawake   sehemu ya  kazi   wakati wa  mafunzo ya  siku  moja  yaliofanyika   katika  ukumbi wa  chekechea wa  Kanisa  Katoliki  Jimbo la  Mpanda  na kufunguliwa na   Mwenyekiti wa  CWT   wilaya ya  Mpanda   Jumanne  Msomba.
Mafunzo  hayo ya  siku  moja  yaliondaliwa na  CWT  Wilaya ya  Mpanda  yalikuwa na  lengo la kuwaelimisha walimu viongozi wa   wanawake   sehemu ya kazi  ili  waweze  kutmbua  haki zao na kuzilinda pamoja na kupatiwa  mafunzo ya  ujasiliamali ili wajikomboe  kiuchumi .
Baadhi ya  walimu hao wanawake walieleza kuwa  kumekuwepo  na  tabia kwa  waajiri  kuwakatalia  kuwapa uhamisho  walimu wa wanawake      pindi  wanapokuwa  wamafunga  ndoa  wanapo omba  uhamisho wa kuwafuata wenzi wao .
Mmoja  wa  Walimu hao   Siwezi   Machulo alieleza  kuwa  ndoa  nyingi  za Walimu wanawake zimevunjika kutokana  na walimu  wanawake  kunyima  uhamisho wa kuwafuata  wenzi wao hasa wanao   kuwa  nje ya  Mkoa wa Katavi .
 Alifafanua  kuwa  mwajiri  amekuwa akiwanyima  uhamisho wa kuwafuata  wenzi wao kwa kile ambacho  amekuwa akidai kuwa  mwalimu  anaetaka kuhamishwa kumfuata  mwenzi wake  hawezi kuhamishwa  hadi hapo  atakapo  kuwa  amepata  mwalimu  mwingine wa kubadilishana  nae huko anakotaka kuhamia wakati sio utaratibu wa  Sheria ya  ndoa .
  Walimu hao wa  kitengo  cha  Wanawake  sehemu ya  kazi wamelalamikia  pia tabia ya  mwajiri wao  ya kuwatengenezea majeneza yaliochini ya  kiwango walimu  ambao wanao kuwa wamefarik Duniai tofauti na watumishi wa idara  nyingine  wanapokuwa wamefariki  majeneza yao yanakuwa na kiwango chenye ubora .
 Awali  akifungua  mafunzo hayo  Mwenyekiti wa CWT   Wilaya ya Mpanda   Jumanne  Msomba  aliwataka walimu  kufanya  kazi kwa kufuata  taratibu za kazi  katika  utumishi wao .
 Alisema   walimu  viongozi wa  wanawake  sehemu ya  kazi wanao wajibu   wa kuwaelimisha  walimu  wafahamu  haki zao za  msingi  kama vile uhamisho wa kuwafuata wenzi wao ,likizo kupandishwa madaraja na kurekebishiwa  mishahara.
Nae  Kaimu  Katibu wa CWT  Wilaya ya  Mpanda   Masanja  Manyanga  alisema kuwa hakuna  sheria  yoyote wala  utaratibu unae mvuia mtu aliyefunga  ndoa kumfuata mwenzi wake kwa kisingizio cha  mpaka  awe  na mtu wa kubadilishana  nae .
 Alisema uwo ni unyanyansaji wa kijinsia hivyo walimu wenye  malalamiko hayo wayafikishe CWT ili waweze kuona  namna ya kushusghulikia  kwa mwajiri anaefanya hivyo .
Kuhusu  majeneza ya Walimu yanayotengenezwa chini ya kiwango alisema ni jukumu la mwajiri kugharamia gharama za mtumishi hivyo sio  swala la hiari  bali ni  haki ya  mtumishi  hivyo pindi wanapoona mwalimu mwenzao  ametengenezewa jeneza lililo chini ya kiwango walikatae kulipokea .

No comments:

Post a Comment