Na Walter Mgulucuma
Katavi Yetu Blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kukamatwa wakiwa wanatoa fedha Tawi la NMB Mpanda kiasi cha shilingi milioni 3,680.000 wakiwa na kadi za ATM 19 mali za watu tofauti pamoja na Namba za siri za kadi hizo .
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Damasi Nyanda aliwaambia Waandisi wa Habari kuwa watuumiwa hao watatu walikamatwa hapo jana majira ya saa tatu usiku katika Tawi la NMB Mpanda .
watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa kwa kuwa umepelelezi bado unaendelea walikamatwa na Askari wa Jeshi la polisi waliokuwa wakilinda Benki hiyo.
Nyanda alieleza watumiwa walikamatwa baada ya Askari polisi kuwatilia mashaka kutokana na kuwaona wakiwa wamekaa muda mrefu kwenye chumba cha mashine ya kutolea feda .
Baada ya kuwatilia mashaka polisi waliingia ndani ya chumba hicho na kuwakuta watumiwa hao wakiwa wanaendelea kutowa fedha katika mashine tatu zilizomo kwenye mashine za kutolea fedha .
Kaimu Kamanda alieleza ndipo Askari polisi walipoamua kuwapekua watuumiwa na waliweza kuwakuta wakiwa na kadi za ATM 19 mali za watu tofauti pamoja na Namba za siri za kadi izo na walikuwa tayari wameisha towa kiasi cha fedha tasilimu silingi milioni 3,680,000.
Alizitaja Namba za Kadi za ATM walizokamatwa nazo watuumiwa kuwa AC
61908000058,AC 61902403196,AC61902400417,AC61908000427,AC
61902240100,AC 61908000237,AC 61902400518 AC 61910000645, AC
61910004240,AC 61908000609 AC 61902403168.
Kaimu kamanda Nyanda alizitaja kadi za ATM nyingine zilizokamatwa kuwa ni zenye namba AC 61910000537,AC 61902402653, AC 61910000250, Ac 61902400818, AC 61908000449,AC1902403219 AC 61910002329 na AC , 70408100131.
Alisema watuhumiwa wanatarajia kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi wa tukio hili utakapokuwa umekamilika na bado watuumiwa wote watatu wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi .
Kaimu kamanda ametowa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kutowa siri kwa watu za namba zao za siri za kadi wanazozitumia za ATM za kwenye Mabenki .
No comments:
Post a Comment