Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu Blog
Mwamlimu Mkuu msaidizi wa shule ya Sekondari Usevya Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi Makonda Ng-onga amefikishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda kwa tuhumma za kumlawiti wanafunzi wake wa kiume wa kidato cha tano ambaejina lakelimehifadhiwa kinyume na maumbile yake .
Mtuhumiwa alifikishwa kizimbani hapo juzi na kusomewa mashita na mwanasheria wa Serikali Mkoa wa Katavi Gregoli Mhagwa mbele ya Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Mpanda Chiganga Ntengwa .
Mwanasheria huyo wa Serikali alidai kuwa mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo hapo Novemba mwaka jana hadi Aprili mwaka huu kwa nyakati tofauti huko katika eneo la shule ya Sekondari ya Usevya Tarafa ya Mpimbwe Wilayani Mlele .
Gregoi l aliiakuiambia mahakama kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo la kumwingilia kinyume na maumbile yake ya kiume mwanafunzi wake wa kidato cha tano wa shule hiyo kwa kutumia nafasi yake ya mkuu wa shule msaidizi .
Alisema Makonda anashitakiwa kwa kosa la kifungu cha sheria Namba 154 kifungu kidogo a sura ya 16 ya sheria ya marekebisho ya sheria ya mwaka 2002.
Mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo baada ya kuwa mwanafunzi huyo anapokuwa amefanya kosa shuleni hivyo hulazimisha kumwingila kinyume cha maumbile yake vinginevyo kama mwanafunzi huyo atakataa amekuwa akimtishia kumfukuza shule .
Mwanasheria wa Serikali baada ya kusomea mashita hayo mthumiwa Makonda alikana kutenda kosa hilo mbele ya Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama hiyo Chiganga Ntengwa .
Hakimu Chiganga aliharisha kesi hiyo hadi hapo june 27 itakapotanjwa tena na mshitakiwa aliweza kupata mdhamana baada ya kutimiza masharti ya amdhamana ambapo alitakiwa kuwa na mdhamini mmoja ambae alisaini hati ya shilingi milioni tatu mahakamani hapo .
Kablayatukio hilo la mtuhumiwa kufikishwa Mahakamani wanafunzi washule hiyo walimkaa mwalimu huyo mbele yaAfisa ElimuwaMkoa wa Katavi Eneresti Hinju kwa kile walichodai kuwa amekuwa akiwafanyia vitendo vya kuwalawiti baadhi ya wanafunzi wavulana wanaosoma katika Sekondarihiyo ya Usevya.
MWISHO
No comments:
Post a Comment