Na Walter Mguluchuma
Katavi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limewakamata Watuhumiwa wane wakiwa wanabunduki ina ya SMG moja ikiwa na Magazine mbili kubwa na ndogo zikiwa na Risasi 86 baada ya kurushiana risasi na Askari wa jeshi la Polisi kabla hawaja kamatwa.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda aliwaambia waandishi wa Habari kuwa tukio hilo lilitokea hapo juzi majira ya saa moja na nusu jioni huko katika Kijiji cha Busongola kambi ya Wakimbizi ya Mishamo Wilaya ya Mpanda.
Aliwataja watuhumiwa hao wane kuwa ni James Amos 28, AMOS Maliyatabu 70, Leoben Kagoma 25 wakazi wa Kijiji cha Busongola na Kulwa Joseph Mkazi wa Kijiji cha Bulamata kambi ya wakimbizi ya Mishamo.
Kaimu Kamanda Damas Nyanda alisema watuhumiwa hao walikamatwa baada ya jeshi la Polisi kupata taarifa za kutoka kwa raia wema kwamba huko katika Kijiji cha Busongola barabara ya nne Kata ya Bulamata makazi ya wakimbizi ya Mishamo kuna watu wanamiliki silaha kinyume cha sheria na wamekuwa wakizitumia kwa ajiri ya kufanyia ujambazi .
Baada ya taarifa hizo jeshi la polisi lilichukua hatua za haraka na kufika kwenye maeneo hayo na kufanya msako nyumbani kwa Amos Maliyatabu na waliweza kukuta nyama ya kiboko ikiwa inapikwa ndani ya sufuria.
Nyanda alieleza kuwa wakati polisi wakiwa wanaendelea na msako waliweza kukutana na watuhumiwa watatu Harumkiza Joshua,Kulwa Joseph na mwenzao mmoja ambae jina lake limehifadhiwa kwa ajiri ya upelelezi.
Watuhimiwa hao walikataa amri ya polisi ya kutaka kuwakamata na ndipo walipoanza kujibishana risasi na askari polisi katika mabishano hayo mtuhumiwa Harumkiza Joshua alipigwa risasi na kufariki Dunia hapo hapo .
Alieleza kuwa polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa Kulwa Joseph pamoja na Bunduki aina ya SMG yenye Namba TX597 1996 na magazine mbili moja kubwa yenye uwezo wa kuhifadhi risasi 45 na ndogo yenye kufifadhi risasi 30 pamoja na risasi 86 zikiwa zimehifadhiwa kwenye mfuko wa salifeti ambapo mwenzao mmoja aliweza kufanikiwa kutoroka na kutokomea porini huku akiwa na silaha yake bunduki nab ado anaendelea kutafutwa .
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi alisema katika eneo hilo la mabishano ya risasi polisi waliweza kukuta pikipiki moja yenye namba za usajiri T.241CKZ aina ya SANLG na kitambulisho cha kupigia kura vilivyobainika kuwa ni mali ya mtuhumiwa aliyetoroka.
Katika uchunguzi wa awali jeshi la polisi limebaini kuwa watuhumiwa hao wamekuwa wakijihusisha kwenye matukio mbalimbali yaliokuwa yakitokea ya unyang-anyi wa kutumia silaha na ujangili.
Mpaka sasa jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa wane ambao ni James Amos , Amos Maliyatabu ,Leoben Kagoma na Kulwa Joseph ambao wanatarajia kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika ,pia mwili wa marehemu huyo baada ya tukio hilo ulifikishwa katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda na baada ya kufanyiwa uchunguzi ulikabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajiri ya mazishi.
Kaimu kamanda Nyanda ametowa shukrani kwa wananchi wa Katavi kwa ushirikiano wanaoendelea kutowa kwa jeshi la polisi kwa kufanikisha ukamatwaji wa silaha na watuhumiwa hao aidha amewahiza wananchi ambao wanamiliki silaha kinyume cha sheria kusalimisha silaha zao katika vituo vya polisi vilivyo karibu nao.
0 comments:
Post a Comment