Wednesday, April 27, 2016

POLISI WAKAMATA BUNDUKI YA KIVITA AINA YA SMG NA RISASI 86 MAGAZINE MBILI BAADA YA KURUSHIANA RISASI NA WATUHUMIWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

  Na  Walter  Mguluchuma
  Katavi 
Jeshi  la  Polisi  Mkoa wa Katavi limewakamata  Watuhumiwa wane wakiwa  wanabunduki  ina ya  SMG   moja   ikiwa na Magazine mbili kubwa na ndogo zikiwa na Risasi 86 baada ya kurushiana  risasi na Askari wa  jeshi la Polisi kabla hawaja  kamatwa.

Kaimu  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi  Damas  Nyanda  aliwaambia waandishi wa  Habari kuwa tukio hilo lilitokea   hapo juzi  majira ya saa moja na nusu jioni   huko  katika Kijiji cha  Busongola    kambi ya Wakimbizi ya  Mishamo Wilaya ya  Mpanda.

Aliwataja watuhumiwa hao wane kuwa ni   James  Amos  28, AMOS  Maliyatabu  70, Leoben  Kagoma 25 wakazi wa Kijiji cha  Busongola  na  Kulwa Joseph   Mkazi wa Kijiji cha  Bulamata  kambi ya wakimbizi ya Mishamo.

Kaimu  Kamanda  Damas  Nyanda  alisema watuhumiwa hao walikamatwa  baada ya jeshi la Polisi  kupata  taarifa za   kutoka kwa raia  wema  kwamba huko  katika   Kijiji cha Busongola   barabara ya  nne  Kata ya  Bulamata  makazi ya wakimbizi ya Mishamo kuna watu   wanamiliki  silaha  kinyume cha  sheria  na wamekuwa  wakizitumia kwa ajiri ya kufanyia ujambazi .

Baada ya taarifa  hizo  jeshi la polisi  lilichukua  hatua za haraka  na kufika  kwenye maeneo   hayo na  kufanya msako  nyumbani kwa  Amos  Maliyatabu  na waliweza  kukuta  nyama ya kiboko ikiwa inapikwa ndani ya  sufuria.
Nyanda  alieleza kuwa  wakati polisi wakiwa wanaendelea na msako  waliweza kukutana na watuhumiwa  watatu  Harumkiza   Joshua,Kulwa Joseph na  mwenzao mmoja  ambae  jina lake limehifadhiwa kwa ajiri ya upelelezi.

 Watuhimiwa  hao walikataa amri ya polisi  ya kutaka kuwakamata  na  ndipo walipoanza kujibishana risasi na askari polisi  katika mabishano hayo  mtuhumiwa   Harumkiza Joshua  alipigwa risasi na kufariki Dunia  hapo hapo .

Alieleza kuwa   polisi  walifanikiwa kumkamata  mtuhumiwa  Kulwa  Joseph  pamoja na Bunduki aina ya  SMG  yenye  Namba   TX597   1996 na magazine  mbili moja kubwa yenye  uwezo wa  kuhifadhi risasi 45 na  ndogo yenye kufifadhi risasi 30 pamoja na risasi 86 zikiwa zimehifadhiwa kwenye mfuko wa salifeti  ambapo mwenzao mmoja  aliweza kufanikiwa kutoroka na kutokomea porini  huku akiwa na silaha yake bunduki  nab ado anaendelea kutafutwa .

Kaimu  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi  alisema katika eneo hilo la mabishano ya risasi  polisi waliweza  kukuta   pikipiki  moja  yenye   namba  za usajiri  T.241CKZ aina ya SANLG na kitambulisho  cha kupigia kura  vilivyobainika  kuwa ni mali  ya  mtuhumiwa  aliyetoroka.

Katika    uchunguzi wa  awali  jeshi la polisi  limebaini  kuwa  watuhumiwa   hao wamekuwa  wakijihusisha  kwenye matukio mbalimbali  yaliokuwa yakitokea ya unyang-anyi wa kutumia silaha  na ujangili.

Mpaka  sasa jeshi hilo  linawashikilia  watuhumiwa wane  ambao ni  James  Amos , Amos  Maliyatabu ,Leoben Kagoma  na  Kulwa Joseph ambao  wanatarajia  kufikishwa  mahakamani  baada ya upelelezi kukamilika ,pia  mwili wa  marehemu huyo  baada ya tukio hilo  ulifikishwa katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda  na baada ya kufanyiwa uchunguzi  ulikabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajiri ya mazishi.
Kaimu  kamanda  Nyanda ametowa  shukrani kwa wananchi wa Katavi kwa ushirikiano wanaoendelea kutowa kwa jeshi la polisi  kwa  kufanikisha  ukamatwaji wa silaha na  watuhumiwa hao  aidha amewahiza  wananchi ambao wanamiliki  silaha  kinyume  cha  sheria  kusalimisha silaha zao  katika  vituo vya polisi  vilivyo karibu nao.

No comments:

Post a Comment