Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mkazi wa Mtaa wa Mji wa Zamani Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi Shukuru Korongo 32 amefariki Dunia baada ya kupigwa na mwenzake baada ya kutokea ugomvi wa kugombea Viroba vya pombe aina ya zed wakati wa sherehe za kumtoa nje mtoto wa jirani yao.
Mwenyekiti wa Mtaa huo Magreti John Kitunguru aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa tukio hilo lilitokea hapo juzi majira ya saa tano usiku katika mtaa huo wa Mji wa zamani .
Mwenyekiti huyo wa mtaa alisema siku hiyo ya tukio marehemu alikuwa na rafiki yake aitwaye Pisikitu Maiko wakiwa nyumbani kwa jirani yao ambae alikuwa amewaalika katika sherehe za kumtoa mtoto wake nje.
Alisema ndipo marehemu alipopewa viroba vya Zed na mwandaaji wa sherehe hizo ili aweze kuwagawia watu waliokuwepo kwenye sherehe hizo za kumtoa mtoto nje .
Alieleza ndipo Pisikitu alipoanza kumtuhumu marehemu kuwa viroba alivyowagawia ni vichache hivyo alimtaka amwongezee viroba vingine kwani alipewa vingi na amevificha .
Hata hivyo marehemu alikataa kata kata kumwongezea viroba vingine kwa kile alichodai kuwa viroba alivyobaki navyo vinamtosha yeye mwenyewe kuvinywa na kuvimaliza .
Mwenyekiti huyo wa mtaa alieleza kuwa ndupo baada ya hapo ndipo ulianza ugomvi wa kupigana baina ya Marehemu na Pisikiti hadi hapo marehemu alipozidiwa na kuanguka chini hari ambayo ilipelekea wambebe marehemu hadi chumbani kwake na ilipofika majira ya saa 12 ya arufajili mama mzazi wa Shukuru alimkuta akiwa ameisha fariki Dunia.
Ndipo mama wa marehemu alipotoa taarifa kwa uongozi wa serikali ya mtaa ambao walifika kwenye eneo hilo na kasha walitowa taarifa kwa jeshi la polisi ambao walifika kwenye eneo hilo.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda amethibitisha kutokea kwa kifo hicho katika mtaa wa Mji wa zamani hapo juzi na alisema mwili wa marehemu upo katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya wilaya ya Mpanda kwa ajiri ya uchunguzi wa kidaktari.
Na Jeshi la polisi linamshikilia Pasikiti Maiko kwa mahojiano zaidi kuhusiana na kifo hicho wakati jeshi hilo likiwa linaendelea na upelelezi zaidi .
No comments:
Post a Comment