Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mtoto Mariamu Malungo 9 Mkazi wa Kijiji cha Kapanga Kata ya Katuma Wilaya ya Mpanda amekutwa akiwa ameuwawa kikatili kwa kuchomwa na kisu kifuani baada ya kubakwa na mtu asiye julikana wakati akiwa analinda Gendele wasile mazao kwenye shamba la Bibi yake.
Kwa mujibu wa Babu wa Marehemu Mahela Manyanda ambae ni Katibu wa Chama cha wafugaji wa Mkoa wa Katavi tukio hilo la mauwaji ya kikatili na yakusikitisha lilitokea hapo juzi majira ya saa tisa mchana Kijijini hapo .
Aliwaambia jana waandishi wa Habari Kijijini hapo kuwa siku hiyo ya tukio marehemu alitumwa majira ya saa tatu asubuhi na Bibi yake ambae walikuwa wakiishi nae kwenda shambani kulinda mazao yasiliwe na Ngedele.
Alisema kuwa Mariamu alikubali agizo hilo la bibi yake na alikwenda shambani kwa bibi yake kulinda mazao hayo huku akiwa peke yake .
Manyanda aliendelea kuelezailipofika muda wa saa saba bibi yake alimwagiza mjuu kuu mwingine aende shambani akamwite Mariamu kwa ajiri ya kula mlo wa mchana ambao ulikuwa upo tayari .
Ailisema baada ya kufika shambani hakuweza kumpa Maremu aliambayo ilimfanya arudu nyumbani kutowa taarifa kwa bibi yake ambae nae alielekea huko shambani kwa lengo la kumtafuta hata hivyo hakuweza kumpata hari ambayo ilimfanya apate shaka na kurudi nyumbani .
Baada ya kurudi nyumbani alikwenda kwenye ofisi za kijiji kutowa taarifa aliambayo iliwafanya viongozi wa Kijiji wapige mbiu na watu walikusanyika ofisini hapo .
Alisema baada ya wananchi kukusanyika hapo walikubaliana kuanza kufanya msako wa kumtafuta mototo huyo na ndipo walipokuwa kwenye dalili za kukata tama waliona mburuzo ukiwa unaelekea kichakani .
Na ndipo walipoweza kuona mwili wa marehemu Mariamu ukiwa kwenye kichaka karibu na mto na walipouchunguza walikuta marehemu akiwa amebakwa na kuharibiwa vibaya sehemu za siri huku akiwa amechomwa vifu viwili kifuani kwake huku akiwa amefariki Dunia.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limethitisha kutokea kwa mauwaji hayo na mpaka sasa wanamshikilia mfugaji mmoja wa mifugo kuhusiana na tukio hilo
No comments:
Post a Comment