Na Walter Mguluchuma
Katavi
Jumla ya idadi ya silaha 11 zimesalimishwa Mkoani Katavi katika zoezi linaloendelea la uhakiki wa sila katika Mkoa wa Katavi na mpaka sasa silaha 76 zimeisha akikiwa kati ya silaha 193 zinazomilikiwa kiharali .
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda aliwaambia waandishi wa Habari jana kuwa zoezi hilo la uhakiki wa silaha katika Mkoa huo lilianza machi 21 na litamalizika Mei 20 mwaka huu.
Kaimu Kamanda Nyanda alisema aina ya silaha aina ya Short Gun zinazomilikiwa kihalali 123 zilizohakikiwa mpaka sasa ni 48 Pistol zinazomilikiwa kiharali ni 40 na zilizohakikiwa ni 16.
Idadi ya bunduki aina ya Rafle zinazomilikiwa kihalali Mkoani hapa ni 30 ambazo zimehakikiwa ni kumi na mbili ambazo hazijahakikiwa ni bunduki kumi na nane na Bunduki kumi na moja aina ya Gobore zimesalimishwa na watu waliokuwa wakizimiliki visivyo harali.
Kaimu Kamanda alisema kasi ya watu wanaomiliki silaha imekuwa sio ya kuridhisha kutokana na wanaomiliki silaha hizo kuwa wamejitokeza wachache kwenda kuhakiki silaha ambapo mpaka sasa ni asilimia 39.3 ndio zimehakikiwa huku ambazo zikiwa hazija hakikiwa zikiwa ni asilimia 60.6.
Aidha kwa Fambao wananchi ambao wanamiliki silaha isivyo halali wanatakiwa kuzisalimisha mara moja katika vituo vya polisi vilivyopo karibu ama kwa viongozi wao wa Serikali za mitaa.
Alisema kwa wale ambao waliorithishwa silaha na ndugu zao baada ya mmiliki kufariki wahakikishe wanazisalimisha polisi na endapo watazihitaji wasisite kufuata utaratibu wa kisheria wa kumiliki silaha.
Pia Kaimu Kamanda Nyanda ametowa onyo kali kwa baadhi ya wananchi wanaomiliki silaha kutoziazimisha kwa makampuni ya ulinzi wala kwa watu wengine badala yake wazitumie silaha hizo kwa mujibu wa taratibu na sheria elekezwa.
No comments:
Post a Comment