Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Monjor Genenal Mstaafu Paphael Luhuga amekemea tabia ambayo imeanza kuenea Mkoani Katavi na kwenye baadhi ya Mikoa hapa nchini ya wagonjwa kuwapiga madaktari kwani kitendo hicho si cha kistaarabu .
Mkuu huyo wa Mkoa wa Katavi alitowa kauli hiyo hapo juzi wakati alipokuwa akizungumza na wataalamu mbalimbali wa kada ya afya wa Hospitali ya Wilaya Mpanda wakati wa ziara aliyoifanya ya kuangalia hari ya Hospitali hiyo.
Alisema tabia ambayo imeanza kuenea hivi karibuni kwa wagonjwa kuwapiga madaktari na wauguzi sio wakistaabu na lazima ikomeshwe kwani watu mishi wa afya lazima waheshime na waachwe wafanye kazi zao .
Mkuu huyo wa Mkoa alieleza kuwa kazi ya kuwahudumia wagonjwa inaathari sana hivyo tuwape moyo wa kujituma madaktari na wauguzi ili waendelee kutowa huduma .
Monjor Genelal Muhuga alieleza matatizo yanayo kabili hospitali hiyo ya Wilaya ya Mpanda yanafanana na matatizo yaliopo kwenye hospitali nyingi zilizopo hapa Nchini .
Alizitaja baadhi ya changamoto zinazozikabili hospitali kuwa ni kuwa bajeti ndogo ambayo haikidhi mahitaji uhaba wa vifaa tiba na uchakavu wa majengo na uchache wa magari ya usafi na serikali imeisha ziona changamoto hizo na tayari wameisha anza kuchukua hatua .
Alifafanua kuwa Serikali imepanga kwenye Bajeti hii kutenga kiasi cha shilingi bilioni mbili kwa ajiri ya ujenzi wa Hospitali ya Mkoa wa Katavi na itakapo kamilika itapunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali hiyo ya Wilaya ya Mpanda inayotumika kwa sasa kama hospitali ya Mkoa wa Katavi .
Hivi kribuni kulitokea matukio matatu ya watumishi wa afya wa Mkoa wa Katavi kupingwa tukio la kwanza muuguzi mmoja katika wodi ya wazazi katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda alipigwa na mgonjwa na tukio jingine lilitokea katika Zahanati ya Kapalamsenga ambapo wananchi walitaka kuandamana huku wakiwa na mwili wa marehemu ili kumpelekea mganga wa zahanati hiyo alale na mwili wa marehemu nyumbani kwake na tukio la tatu lilitokea katika zahanati ya Simbesa ambapo mwenyekiti wa kijiji alipiga mganga wa zahanati hiyo.
Katika taarifa iliyosomwa mbele ya Mkuu huyo wa Mkoa na mratibu wa ukimwi wa Wilaya ya Mpanda dK Benald Kamande kwa niaba Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda alieleza kuwa katika utekelezaji wa shughuli za hospitali hiyo ya Wilaya imejiwekea malengo mbalimbali .
Aliyataja malengo hayo kuwa ni kutowa elimu ili kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi,kuhakikisha dawa na vifaa tiba katika hospitali vinapatikana ili kukidhi mahitaji.
Dk Kamande alieleza lengo jingine ni kuboresha utoaji na upatikanaji wa huduma za afya katika kiwango kinachokubalika na kuimalisha huduma za dharula na upasuaji kwa akina mama wenye vizazi pingamizi OBSTRUCTED LABOUR ili kupunguza vifo na magonjwa ya milipuko.
No comments:
Post a Comment