Home » » RC AKEMEA TABIA YA KUPIGWA KWA MADAKTARI NA WAUGUZI

RC AKEMEA TABIA YA KUPIGWA KWA MADAKTARI NA WAUGUZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na  Walter  Mguluchuma 
Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Monjor  Genenal Mstaafu  Paphael  Luhuga  amekemea  tabia ambayo imeanza kuenea Mkoani Katavi na kwenye  baadhi ya  Mikoa  hapa nchini ya  wagonjwa kuwapiga madaktari  kwani kitendo hicho si cha kistaarabu .
Mkuu  huyo wa  Mkoa wa Katavi  alitowa  kauli  hiyo  hapo juzi wakati alipokuwa  akizungumza na wataalamu  mbalimbali wa  kada  ya  afya   wa  Hospitali ya  Wilaya  Mpanda wakati  wa  ziara aliyoifanya  ya kuangalia  hari ya Hospitali  hiyo.
Alisema  tabia  ambayo  imeanza kuenea  hivi  karibuni kwa wagonjwa kuwapiga  madaktari na wauguzi sio wakistaabu  na  lazima  ikomeshwe  kwani watu mishi wa afya  lazima  waheshime   na waachwe wafanye   kazi    zao .
Mkuu  huyo wa  Mkoa  alieleza  kuwa  kazi ya  kuwahudumia  wagonjwa  inaathari sana   hivyo   tuwape  moyo wa kujituma madaktari na wauguzi   ili waendelee  kutowa  huduma .
Monjor  Genelal  Muhuga  alieleza  matatizo  yanayo  kabili  hospitali  hiyo ya  Wilaya  ya  Mpanda  yanafanana  na  matatizo  yaliopo  kwenye  hospitali nyingi  zilizopo  hapa  Nchini .
 Alizitaja  baadhi ya  changamoto zinazozikabili  hospitali  kuwa   ni kuwa  bajeti  ndogo ambayo haikidhi mahitaji  uhaba wa vifaa  tiba  na  uchakavu wa  majengo   na  uchache wa magari ya usafi na  serikali imeisha ziona  changamoto hizo na  tayari  wameisha  anza kuchukua  hatua .
 Alifafanua kuwa  Serikali  imepanga  kwenye  Bajeti  hii kutenga kiasi cha shilingi  bilioni  mbili kwa ajiri ya ujenzi wa  Hospitali ya Mkoa wa Katavi  na itakapo kamilika itapunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali  hiyo ya Wilaya ya Mpanda  inayotumika  kwa sasa kama  hospitali ya Mkoa wa Katavi .
Hivi  kribuni kulitokea  matukio matatu ya watumishi wa afya wa Mkoa wa Katavi kupingwa tukio la kwanza  muuguzi  mmoja katika wodi ya wazazi katika  hospitali ya Wilaya ya Mpanda alipigwa na mgonjwa na tukio jingine lilitokea  katika Zahanati ya Kapalamsenga  ambapo wananchi walitaka kuandamana  huku wakiwa na mwili wa marehemu ili kumpelekea  mganga wa  zahanati hiyo alale  na  mwili wa marehemu nyumbani kwake na tukio la tatu lilitokea katika  zahanati ya Simbesa ambapo mwenyekiti wa kijiji alipiga  mganga wa zahanati hiyo.
 Katika  taarifa  iliyosomwa  mbele ya Mkuu huyo wa Mkoa  na  mratibu wa ukimwi wa Wilaya ya  Mpanda dK  Benald  Kamande kwa niaba   Kaimu  Mganga  Mkuu wa Halmashauri ya  Wilaya ya  Mpanda  alieleza kuwa  katika  utekelezaji  wa  shughuli  za  hospitali hiyo  ya  Wilaya  imejiwekea   malengo mbalimbali .
Aliyataja  malengo  hayo kuwa ni  kutowa  elimu  ili kupunguza  maambukizi  ya virusi  vya ukimwi,kuhakikisha  dawa na vifaa  tiba  katika  hospitali  vinapatikana  ili kukidhi mahitaji.
Dk  Kamande  alieleza  lengo jingine ni  kuboresha  utoaji na upatikanaji  wa huduma  za afya  katika  kiwango  kinachokubalika na kuimalisha  huduma za dharula  na upasuaji kwa akina  mama  wenye  vizazi pingamizi OBSTRUCTED  LABOUR   ili kupunguza vifo na  magonjwa ya  milipuko.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa