Thursday, April 7, 2016

HOSPITALI YA WILAYA YA MPANDA INAKABILIWA NA TATIZO LA UPUNGUFU WA WATUMISHI ZAIDI YA 150

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

       N  a  Walter  Mguluchuma
              Katavi
Hospitali ya  Wilaya  ya Mpanda  Mkoa wa  Katavi  ilioanzishwa mnamo  mwaka  1957 kama   kituo cha  Afya  na  baadaye  ilipewa    hadhi  kuwa  Hospitali ya Wilaya   mwaka  1977 inakabiliwa na  tatizo la upungufu wa  watumishi 157 wa kada  mbalimbali wa afya  na uchakavu  mkubwa wa majengo .
Hayo  yalisemwa  hapo  juzi  kwenye  risala ya  watumishi  wa Hospitali  hiyo  iliyosomwa  na  Mratibu wa kuzuia  ukimwi wa Wilaya ya  Mpanda   Dk  Benald  Kamande  mbele ya  Mkuu wa  Mkoa wa  Katavi Monjor Genelali   msitaafu  Raphae  Luhuga  wakati   ziara  yake ya kutembelea na kukagua  Hospitali  hiyo.
  Alisema  Hospitali hiyo  ya  Wilaya  ya  Mpanda  inakabiliwa  na  changamoto ya   upungufu wa watumishi wa  afya wa  kada  mbalimbali   ambapo mpaka  sasa inao watumishi  wapatao  261 wakati mahitaji ya watumishi ni  386 hivyo wanaupungufu  wa  watumishi 157 wa  kada  mbalimbali  wa  afya.
Hospitali  hiyo  ya  Wilaya  kiujumla  imekuwa  na  uhaba  wa dawa  wakati wote  hali  hii  inatokana  na  ufinyu wa  bajeti  na ndio  hospitali inayotowa  huduma  kwa kuhudumia watu wa Mkoa  mzima  kutokana  na  Mkoa  kutokuwa na  Hospitali ya Mkoa  huku  bajeti yake  ikiwa ni ya hospitali ya  Wilaya .
  DK  Kamande  alieleza  Hospitali  hiyo  pia  inakabiliwa na  uchakavu  miundo  mbinu   katika   Hospitali  kama  vile  majengo  ambayo mengi yalijengwa toka  mwaka  1957 na  majengo ya  mwisho yalijengwa  mwaka 1977.
 Changamoto  nyingine  ni  fedha  za kuendeshea  huduma  za  afya  kutofika  kwa wakati hari  ambayo imekuwa ikisababisha baadhi ya  shughuli kutofanyika kwa wakati  na uchakavu wa  magari ..
Dk  Kamande  alieleza  utatuzi wa  changamoto  hizo unendelea   ambapo  Halmashauri inaendelea  kupata  watumishi  wapya ingawa  hawaja   toshereza  kulingana  na  mahitaji ya  ikama .
 Hospitali   imefungua    mfumo  wa   Kielectroniki  wa  kukusanya   mapato  ili kuongeza   tija  ya ukusanyaji  toka  mwezi  Desemba  2015 na  makusanyo yameanza kuongezeka  kutoka   Tsh 180 000   hadi   kufikia   Tsh  600 000 kwa mwezi alieleza  msoma  risala  huyo.
Mkuu wa  Mkoa  Monjor  Jenelali  Mstaafu  Raphael  Luhuga  alikri  kwa hospitali kuelemewa na  mzigo wa kuhudumia wagonjwa wa  Mkoa  mzima wa Katavi wakati  Hospitali  hiyo  inahudumiwa  na   Halmashauri  moja tuu.
  Alisema   Mkoa  umetenga  kwenye  bajeti hii ya  fedha  kiasi  cha  shilingi  bilioni  mbili kwa  ajiri ya  ujenzi wa  Hospitali ya  Mkoa  hari  ambayo  itaipunguzia  hospitali  hiyo  mzigo .

Pia  aliwapongeza watumishi wa hospitali hiyo kwa kufanya  kazi bila  kujali mazingira wanayofanyia  kazi na  amewataka  waendelee kufanya  kazi kwa bidii kubwa na kwauadilifu na watu wawaache  watumishi wa afya wafanye kazi bilakugubudhiwa na watu.

No comments:

Post a Comment