Na Walter Mguluchuma
Katavi
Waislam wa Mpanda wamefanya maombi maalumu kwa ajiri ya kumwombea Rais John Magufuli na Shekh Mkuu wa Tanzania Shehk Abubakar Zuberi wawe na afya njema na Taifa la Tanzania lidizi kuwa na amani .
Maombi hayo maalumu yalifanyika hivi karibuni wakati wa maadhimisho wa kuzaliwa kwa mtume Muhamad S.a.w yaliofanyika katika msikiti wa Aruhmmani katika mtaa wa Nsemlwa Kichangani mjini Mpanda.
Shekh Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Shekh Akilimali ndiye aliyeongoza maombi hayo ambayo pia yaliuzuriwa na na shehk Ramadhani Rashid shekh wa Wilaya ya Tabora ambae alimwakilisha shekh Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
Kwenye maombi hayo shekh Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alieleza kuwa Nchi yetu inahitaji amani huku viongozi wetu wakiwa na afya njema ,busara na uadilifu mkubwa ili waweze kuleta maendeleo ya Taifa.
Aliomba mwenyezi mungu atie Baraka zake kwa viongozi hao wa Taifa na kwa wasaidizi wao ili amani yetu na usitawi wa nchi yetu uzidi kuimalika .
Nae mratibu wa maombi hayo Shekh Idd Mvano alisema maombi hayo yamekuwa ni yakistoria katika Mkoa wa Katavi na yakipekee kwa kuhudhuriwa na Waislaam wengi na viongozi wakuu wa Bakwata wa mikoa miwili ya jirani ya Tabora na Rukwa na wenyeji Katavi na aliomba watu waendelee kudumisha mshikamano huo kwa masilahi ya Watanzania.
Mwakilishi wa Shekh wa Mkoa wa Tabora Shehk Ramadhani Rashid aliwataka viongozi wa dini wajiepushe na migogoro na wazidi kuimalisha mshikamano .
Alisisitiza kuwa uongozi ni dhamana hivyo viongozi wote waliochaguliwa wakiepushe na kiburi kwa watu wao wanao waongoza bila kujali itikadi za dini na vyama vya siasa.
Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa
No comments:
Post a Comment