Tuesday, April 5, 2016

JELA MIAKA 23 KWA KUVUNJA NA KUIBA KWA AFISA MIPANGO WA HALMASHAURI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

    Na  Walter  Mguluchuma

   Katavi
M ahakama ya  Wilaya  ya Mlele  Mkoa  wa  Katavi  imemuhukumu  Omary  Ally  20  kifungo  cha  miaka   23 jela  baada ya kupatikana  na   kosa  la   kuvunja na  kuiba  nyumbani kwa  Afisa  mipango  wa  Halmashauri ya  Wilaya ya  Mlele.
Hukumu hiyo ilitolewa  hapa  jana  na  Hakimu  Mkazi wa  Mahakama ya Wilaya ya  Mlele   Teothimu  Swai baada ya  mshitakiwa kukili makosa  mawili aliyosomewa mahakamani  hapo ya kuiba  na kuvunja.
  Awali  katika  kesi  hiyo  mwendesha  mashitaka  Inspekita wa  jeshi  la  Polisi   Baraka  Hongela  alidai  mahakamani  hapo kuwa  mtuhumiwa  alitenda kosa  hilo  hapo  machi  29  mwaka huu majira ya saa tisa usiku.
Siku  hiyo  ya  tukio  mtuhumiwa alivunja  nyumba ya  afisa  mipango wa Halmashauri ya  Wilaya ya Mlele  Afred  Sungura na  kasha  aliiba    laputopu  moja .
  Mshitakiwa  huyo  baada ya kusomewa  mashita  hayo  mawili alikiri  Mahakamani  hapo  kutenda  makosa  hayo kwa makusudi.
Hakimu  Mkazi  Swai  baada ya  mshitakiwa  kukiri makosa  hayo  alimwambia  mshitakiwa  kama  anayosababu  yoyote ya  msingi ya kuishawishi  mahakama impunguzie  adhabu  basi  anapew  nafasi ya kujitete.
 Katika  utetezi  wake mshitakiwa  aliomba  mahakama impunguzie  adhabu  kwakuwa  bado anaumri   mdogo wa miaka  23  maombi hayo  ambayo yalipingwa  vikari na  mwendesha  mashitaka    Baraka   Hongela na kuimba  mahakama  itowe   adhabu  kali kwa mshitakiwa ilikukomesha watu wengine  wenye  tabia  kama  hiyo.
Hakimu   Swai baada ya kusikia tetezi  huo aliiambia  mahakama  kuwa   mshitakiwa  ameshindwa kutowa   sababu za  msingi za kuishawishi  mahakama  impunguzie  adhabu  hivyo  mahakama imemuhukumu  mshitakiwa kutumikia  jela kifungo  cha miaka  23  jela.

No comments:

Post a Comment