Na Walter Mguluchuma
Katavi
M ahakama ya Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi imemuhukumu Omary Ally 20 kifungo cha miaka 23 jela baada ya kupatikana na kosa la kuvunja na kuiba nyumbani kwa Afisa mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele.
Hukumu hiyo ilitolewa hapa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mlele Teothimu Swai baada ya mshitakiwa kukili makosa mawili aliyosomewa mahakamani hapo ya kuiba na kuvunja.
Awali katika kesi hiyo mwendesha mashitaka Inspekita wa jeshi la Polisi Baraka Hongela alidai mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo hapo machi 29 mwaka huu majira ya saa tisa usiku.
Siku hiyo ya tukio mtuhumiwa alivunja nyumba ya afisa mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Afred Sungura na kasha aliiba laputopu moja .
Mshitakiwa huyo baada ya kusomewa mashita hayo mawili alikiri Mahakamani hapo kutenda makosa hayo kwa makusudi.
Hakimu Mkazi Swai baada ya mshitakiwa kukiri makosa hayo alimwambia mshitakiwa kama anayosababu yoyote ya msingi ya kuishawishi mahakama impunguzie adhabu basi anapew nafasi ya kujitete.
Katika utetezi wake mshitakiwa aliomba mahakama impunguzie adhabu kwakuwa bado anaumri mdogo wa miaka 23 maombi hayo ambayo yalipingwa vikari na mwendesha mashitaka Baraka Hongela na kuimba mahakama itowe adhabu kali kwa mshitakiwa ilikukomesha watu wengine wenye tabia kama hiyo.
Hakimu Swai baada ya kusikia tetezi huo aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa ameshindwa kutowa sababu za msingi za kuishawishi mahakama impunguzie adhabu hivyo mahakama imemuhukumu mshitakiwa kutumikia jela kifungo cha miaka 23 jela.
0 comments:
Post a Comment