Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Serikali inatarajia kuwalipa wananchi wa Mkoa wa Katavi zaidi ya shilingi milioni 600 watu zaidi ya 130 fidia kwa ajiri kupisha ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha rami kutoka Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi hadi Pangale Mkoani Tabora yenye urefu wa kilometa 342 itakayo anza kujengwa hivi karibuni kwa kiwango cha rami.
Hayo yalisemwa hapo jana na Waziri wa Ujenzi uchukuzi na mawasiliano Pro Makame Mbarawa wakati hapo jana wakati alipokuwa akikagua daraja la mto Koga linalounganisha mikoa ya Katavi na Tabora alipokuwa akizungumza na viongozi wa Mikoa ya Katavi na Tabora.
Alisema Serikali ya Tanzania imepata fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa ajiri ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha rami kutoka Mjini Mpanda hadi Pangale Mkoani Tabora yenye urefu wa kilometa 342.
Alieleza fedha kwa ajiri ya ujenzi huo tayari zimefika na ujenzi utakapo anza hauta simama na mtaalamu mshauli amekwisha patikana taratibu za kuwapata wakandarasi tenda itatangazwa wakai wowote kuanzia sasa.
Pro Mbarawa alisema kiasi cha shilingi milioni 606 watalipwa wananchi ambao maeneo yao yatakayopisha ujenzi wa barabara hiyo ambayo itakuwa ni mkombozi kwa wakazi wa Mikoa ya Katavi na Taora.
Alisisitiza kuwa wananchi ambao watakao lipwa fedha hizo za kutisha ujenzi huo ni wale tuu wanaositahili na sivinginevyo.
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi Kanali msitaafu Issa Njiku alimweleza waziri huyo kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na tatizo la baadhi ya sehemu kutokuwa na mawasiliano ya simu hivyo aliomba wizara hiyo kuangalia nanma ya kuboresha huduma hiyo ili iweze kuwafikia wananchi
Pia aliomba barabara ya Inyonga hadi Ilunde yenye urefu wa kilometa 62 ibadilishwe kuto kenye Halmashauri ya Wilaya ya Mlele na kuwa chini ya wakala wa barabara nchini Tan roods.
Akijibu maombi hayo Waziri Mbarawa alisema serikali imeisha ingia mkaba na kampuni ya Haltel ambapo kampuni hiyo tayari imeisha peleka kwenye vijiji 2000 mawasiliano ya simu na kwenye awamu ya pili imepanga kupeleka mawasiliano katika vijiji 1500
0 comments:
Post a Comment