Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima akimshukuru mwenyekiti
wa chama cha msingi cha ushirika cha wakulima wa Tumbaku Mpanda Kati
Bakari Hamis kwa msada uliotolewa na chama hicho cha ushirika wa
madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni saba na nusu kwa ajiri
ya shule za msingi wilayani Mpanda makabidhiano hayo yalifanyika
jana katika ofisi za chama cha Msingi Mpanda Kati
PICHA Na Walter Mguluchuma-Katavi yetu Blog
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Chama cha Msingi cha ushirika cha wakulima wa Tumbaku cha Mpanda kati Mkoa wa Katavi kimetowa msaada wa madawati 100 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni saba kwa ajiri ya kusaidia kupunguza matizo ya upungufu wa madawati katika shule za msingi katika Wilaya ya Mpanda.
Msaada huo ulikabidhiwa jana kwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima katika makabidhiano yaliofanyika katika ofisi za chama cha Msingi Mpanda kati zilizopo katika Mtaa wa Madukani Mjini hapa.
Katika taarifa iliyosomwa wakati wa kukabidhi madawati hayo na Meneja wa chama hicho cha ushirika cha Mpanda Kati Amani Rajabu Athuman mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda ambae pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya mpya ya Tanganyika alisema chama hicho kinakabidhi madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni saba na nusu.
Alisema chama hicho kimechangia madawati hayo ikiwa ni kuunga mkono juhudi ambazo zimekuwa zikifanywa na mkuu huyo wa Wilaya za kuwahamasisha wadau mbalimbali kuchangia sekta ya elimu.
Kutokana na hamasa anayoitowa DC huyo ya kuchangia madawati chama cha msingi mpanda Kati kitaendelea kushilikiana na Serikali katika kuchangia maendeleo kadri uwezo wao.
Meneja huyo wa chama cha msingi alieleza kuwa mbali ya kutowa msaada huo wa madawati chama hicho pia kimeisha changia ujenzi wa ofisi ya Kijiji cha Majalila, nyumba ya mwalimu shule ya Msingi Mpembe, na Ujenzi wa darasa la shule ya Msingi Igalula
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima alishikukuru chamahicho cha Msingi cha Wakulima wa Tumbaku kwa msada huo na kukiomba chama hicho kiendele kutowa misaada na kwenye sekta nyingine kama afya .
Alisema taasisi za mabenki zilizopo katika mkoa wa Katavi nazo zinazo wajibu wa kuchangia mchango wa madawati kama ambavyo walivyofanya chama cha Msingi Mpanda Kati .
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Lauteli Kanoni alisema madawati hayo yatasaidia wanafunzi kusoma vizuri shuleni kwani yatawafanya wasome shule huku wakiwa wamekaa kwenye madaw ati.
0 comments:
Post a Comment