N a Walter Mguluchuma
Katavi
Hospitali ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi ilioanzishwa mnamo mwaka 1957 kama kituo cha Afya na baadaye ilipewa hadhi kuwa Hospitali ya Wilaya mwaka 1977 inakabiliwa na tatizo la upungufu wa watumishi 157 wa kada mbalimbali wa afya na uchakavu mkubwa wa majengo .
Hayo yalisemwa hapo juzi kwenye risala ya watumishi wa Hospitali hiyo iliyosomwa na Mratibu wa kuzuia ukimwi wa Wilaya ya Mpanda Dk Benald Kamande mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Monjor Genelali msitaafu Raphae Luhuga wakati ziara yake ya kutembelea na kukagua Hospitali hiyo.
Alisema Hospitali hiyo ya Wilaya ya Mpanda inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa watumishi wa afya wa kada mbalimbali ambapo mpaka sasa inao watumishi wapatao 261 wakati mahitaji ya watumishi ni 386 hivyo wanaupungufu wa watumishi 157 wa kada mbalimbali wa afya.
Hospitali hiyo ya Wilaya kiujumla imekuwa na uhaba wa dawa wakati wote hali hii inatokana na ufinyu wa bajeti na ndio hospitali inayotowa huduma kwa kuhudumia watu wa Mkoa mzima kutokana na Mkoa kutokuwa na Hospitali ya Mkoa huku bajeti yake ikiwa ni ya hospitali ya Wilaya .
DK Kamande alieleza Hospitali hiyo pia inakabiliwa na uchakavu miundo mbinu katika Hospitali kama vile majengo ambayo mengi yalijengwa toka mwaka 1957 na majengo ya mwisho yalijengwa mwaka 1977.
Changamoto nyingine ni fedha za kuendeshea huduma za afya kutofika kwa wakati hari ambayo imekuwa ikisababisha baadhi ya shughuli kutofanyika kwa wakati na uchakavu wa magari ..
Dk Kamande alieleza utatuzi wa changamoto hizo unendelea ambapo Halmashauri inaendelea kupata watumishi wapya ingawa hawaja toshereza kulingana na mahitaji ya ikama .
Hospitali imefungua mfumo wa Kielectroniki wa kukusanya mapato ili kuongeza tija ya ukusanyaji toka mwezi Desemba 2015 na makusanyo yameanza kuongezeka kutoka Tsh 180 000 hadi kufikia Tsh 600 000 kwa mwezi alieleza msoma risala huyo.
Mkuu wa Mkoa Monjor Jenelali Mstaafu Raphael Luhuga alikri kwa hospitali kuelemewa na mzigo wa kuhudumia wagonjwa wa Mkoa mzima wa Katavi wakati Hospitali hiyo inahudumiwa na Halmashauri moja tuu.
Alisema Mkoa umetenga kwenye bajeti hii ya fedha kiasi cha shilingi bilioni mbili kwa ajiri ya ujenzi wa Hospitali ya Mkoa hari ambayo itaipunguzia hospitali hiyo mzigo .
Pia aliwapongeza watumishi wa hospitali hiyo kwa kufanya kazi bila kujali mazingira wanayofanyia kazi na amewataka waendelee kufanya kazi kwa bidii kubwa na kwauadilifu na watu wawaache watumishi wa afya wafanye kazi bilakugubudhiwa na watu.
0 comments:
Post a Comment