Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Agizo alilolitowa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda
Mkoani Katavi Paza Mwamlima la kupiga marufuku biashara ya kuuza pomba
na kucheza polu na kucheza bao wakati wa kazi limeanza kutelelezwa katika Manispaa ya Mpanda .
Mkuu wa Wilaya hiyo hivi karibuni alitowa agizo la kupiga marufuku uuzaji wa pombe za iana zote katika muda wa kazi katika maeneo yote ya Wilaya ya Mpanda.
Mwamlima mbali ya agizo hilo la kuuza pombe pia alipiga marufuku watu kucheza polu na bao pamoja na watu kuacha kukaa kwenye vijiwe vikiwemo vijiwe vya kawahawa wakati wa muda wa kufanya kazi.
Kufuatia agizo hilo la DC wa Mpanda wafanyabiashara wanao miliki bar na grosali mbalimbali katika manispaa ya Mpanda wametii agizo hilo kwa kuacha kuuza vinywaji vikari muda wa kazi .
Mmoja wa wafanyabiashara mmiliki wa Bar maarufu ya Deluex katika Manispaa hiyo alisema ameanza kuteleleza agizo hilo la Mkuu wa Wilaya kwa kusitisha kuuza vinywaji vikari muda wa kazi .
Alisema huduma ya vinywaji vikari vinaanza kutolewa kwenye bar yake kuanzia saa tisa na nusu ikiwa ni kutekeleza agizo lililotplewa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda .
Miongoni mwa maeneo ambayo yalikuwa yameshamiri uuzaji wa pombe muda wa kazi katika Manipaa ya Mpanda ni mtaa wa Fisi na Mtaa wa Simba ambapo wamiliki wa Grosali na bar katika mitaa hiyo wametii agizo hilo .
Na pia kwenye yale maeneo ambayo watu walikuwa
wakishinda wanacheza polu sasa hivi mchezo huo wanaanza kucheza saa kumi
jioni ikiwa ni katika kuteleza agizo hilo

0 comments:
Post a Comment