Home » » TAASISI YA BENJAMINI MKAPA ITAENDELEA KUIUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO MH. DKT JOHN POMBE MAGUFULI - PINDA

TAASISI YA BENJAMINI MKAPA ITAENDELEA KUIUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO MH. DKT JOHN POMBE MAGUFULI - PINDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na  Walter  Mguluchuma
  Katavi yetu Blog
Waziri Mkuu msitaafu  Mizengo  Pinda   amesema kuwa    Watanzania  wanayoimani  kwamba Taasisi  ya Benjamini Mkapa  itaendelea kuunga  mkono  juhudi  za Rais wa Serikali  ya awamu ya  tano  ya Mhe Dkt John Magufuli  ambae   ameonyesha  dhahiri kuuguswa na suala la kuimarisha afya ya Watanzania.
Pinda alitowa kauli hiyo katika  sherehe ya makabidhiano  ya nyumba 19 za watumishi  wa afya  zilizotolewa na Taasisi hiyo  kwa ajiri ya  Mikoa ya Katavi na Rukwa  zilizofanyika juzi  katika Zahanati ya Kabungu Wilayani Mpanda  ambapo alikuwa mgeni rasmi wa sherehe hizo .
Alisema Taasisi  ya Benjamini Wiliam Mkapa  maarufu Mkapa Foundation  imeweza kuratibu  na  kuwezesha kupatikana  kwa msaada huo  mkubwa  uliogharimu kiasi cha shilingi  Bilioni.
Pinda alieleza  Serikali yetu  kwa kushirikiana  na wadau  mbalimbali  imeendelea  kutekeleza  miradi  ya maendeleo  kwenye sekta ya afya  kwa nia  ya kutekeleza miradi  ya maendeleo  kwenye sekta ya afya  kwa nia ya kuimarisha  afya  za wananchi wake ,mikakati  na  jitihada  za makusudi  zimeendelea  kutekelezwa   katika  kuimarisha  utoaji  wa huduma za utoaji  wa huduma za afya husani  maeneo ya Vijijini.
Licha ya mafanikio  yaliyopatikana Nchi yetu  bado  inakabiliwa  na tatizo  kubwa la  upungufu  wa watumishi  wa afya  hasa maeneo  ya Vijijini nay ale yasiyofikika kwa urahisi  upungufu wa watumishi  wa afya  unakadiliwa  kuwa zaidi  ya asilimia 50 ya mahitaji  katika  vituo vyote vya kutolea huduma ya afya  nchini.
 Alisema  anafarijika  kuona  leo  hii  katika kuimarisha   huduma za afya Wizara  ya afya,Maendeleo  ya jamii  , Wazee na watoto  kwa kushirikiana  na Taasisi  ya Benjamini Wiliam Mkapa  zimesaidia  Mikoa ya Katavi  na Rukwa  katika kuhakikisha  malengo  ya Kitalfa  upatikanaji  wa  watumishi  wa afya  wa kutosha na wenye  sifa  yanafikiwa kwa haraka.
Pinda alieleza kuwa  ukizingatia  huu ni wakati  wa kutekeleza  kaulimbiu ya Hapa kazi  Tu basi anatumia furusa hiyo kwa Halmashauri  kuhakikisha   zinaweka fedha za kutosha na utaratibu  kulingana na miongozo  kuhusu  ukarabati wa majengo zikiwemo pia  nyumba za watumishi iliwaishi katika mazingira mazuri na waweze kutoa huduma bara na stahiki kwa wananchi.
Nae afisa mtendaji mkuu  wa Taasisi  ya Benjamin Wiliam Mkapa DKT  Ellen Senkoro alieza  ujenzi wa nyumba hizo 19 walizokabidhi   umegharimu  jumla ya  shilingi Bilioni 1,394,093,806 ambapo wastani wa nyumba moja umegharimu kiasi cha shilingi Milioni  73.3.
Alisema Taasisi hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 2006 mpaka sasa imeisha  jenga  nyumba 480 kati  Halmashauri 51  nchini  na miongoni mwa nyumba hizo nyumba 30 zimejengwa katika Mikoa ya Katavi
na Rukwa.
Kaimu Mganga mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dkt Naibu Mkongwa  alisema ujenzi wa nyumba hizo utasaidia  kupunguza adha kwa wananchi  ambao  walikuwa  wakikosa huduma  kwa muda  usiku kutokana na waganga na wauguzi  kuishi  mbali na zahanati kwa kuwepo kwa nyumba kutafanya  huduma zipatikane muda wote kwenye vituo ambavyo Taasisi imejenga nyumba .
Muuguzi wa Zahanati ya Kabungu Rose Mpimbe alieleza  kupatikana kwa nyumba ya kuishi  katika Zahanati  kutamwondolea tatizo la kutembea  umbali mrefu kwani allikuwa akiishi kijiji cha  jirani  kilichopo umbali wa kilimeta mbili kutoka kwenye Zahanati .
Alisema  alikuwa analazimika  kuaachwa usiku pindi  kunapokuwa na mgonjwa  na kulazika kutembea kwa miguu umbali huo mida ya usiku kwa ajiri ya kumuudumia mgonjwa ,
Mkazi wa Kijiji cha Kabungu  Frida Futakamba  alisema kukamilika kwa nyumba hiyo kutasaidia  kupatikana muda wote huduma ya  uzazi kwa akina mama kwani wajawazito walikuwa wanalazimika kutafuta wakunga wa jadi kwa ajiri ya kuwasaidia kujifungua kutokana na zahanati yao  kutokuwa na huduma mida ya usiku kutokana na wataalamu kuishi mbali  na Zahanati .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa